Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nayajua Vizuri Maumivu Waliyo Nayo”
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
    • Siku moja alipokuwa akichunga kondoo, Musa aliona jambo lisilo la kawaida, mti fulani wa miiba ulikuwa ukiwaka moto lakini “haukuwa ukiteketea.” (Mstari wa 2) Akitaka kujua kilichokuwa kikifanyika, aliukaribia. Akitumia malaika, Yehova alizungumza na Musa kutoka katikati ya moto: “Usikaribie hapa. Vua viatu vyako kutoka miguuni, kwa sababu mahali ambapo umesimama ni udongo mtakatifu.” (Mstari wa 5) Fikiria hilo, kwa kuwa mti huo wa miiba uliwakilisha kuwapo kwa Mungu, mahali hapo pakawa patakatifu!

  • “Nayajua Vizuri Maumivu Waliyo Nayo”
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
    • Huruma za Mungu zinatupa sababu ya kuwa na tumaini. Kwa msaada wake, sisi wanadamu wasio wakamilifu tunaweza kuwa watakatifu kwa kadiri fulani na kupata kibali chake. (1 Petro 1:15, 16) Mwanamke mmoja Mkristo ambaye amekabiliana na mshuko wa moyo na kuvunjika moyo alifarijiwa na simulizi la Musa kwenye mti wa miiba. Anasema: “Ikiwa Yehova anaweza kufanya ardhi iwe takatifu, basi huenda nina tumaini. Wazo hilo limenisaidia sana.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki