Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Upatanisho (Atonement Day)
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Sehemu Mbalimbali za Siku ya Upatanisho. Haruni alipaswa kuingia katika patakatifu akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya toleo la dhambi na kondoo-dume kwa ajili ya toleo la kuteketeza. (Law 16:3) Katika Siku ya Upatanisho yeye alivua vazi lake la kawaida la kikuhani, akaoga na maji, na kujivika mavazi matakatifu ya kitani. (Law 16:4) Kisha kura zilitupwa na kuhani mkuu juu ya mbuzi wawili (wana-mbuzi wa kiume) waliofanana kabisa katika hali yao ya kuwa timamu na bila waa, waliopatikana kutoka kwa kusanyiko la wana wa Israeli. (Law 16:5, 7) Kuhani mkuu alitupa kura juu yao ili kuamua ni yupi kati yao wawili angetolewa dhabihu kwa Yehova awe toleo la dhambi na ni yupi angeachiliwa nyikani, abebe dhambi zao akiwa ‘mbuzi wa Azazeli.’ (Law 16:8, 9; linganisha 14:1-7; ona AZAZELI.) Kisha yeye alimtoa dhabihu yule fahali mchanga kuwa toleo la dhambi kwa ajili yake mwenyewe na nyumba yake, iliyotia ndani kabila zima la Lawi, ambalo nyumba yake ilikuwa sehemu yalo. (Law 16:6, 11) Kisha alichukua uvumba wenye manukato na chetezo ya moto ikiwa imejaa makaa yenye kuwaka kutoka kwenye madhabahu na kuingia ndani ya pazia, na kupaingia Patakatifu Zaidi. Uvumba ulichomwa katika chumba cha ndani zaidi, ambamo palikuwa na lile sanduku la ushuhuda, lile wingu la uvumba wenye kuchomeka likifunika kifuniko cha lile Sanduku la Agano la dhahabu ambalo juu yake kulikuwa na makerubi wawili waliofanyizwa kwa dhahabu. (Law 16:12, 13; Kut 25:17-22) Tendo hilo lilimfungulia Haruni njia ya baadaye ya kuingia tena akiwa salama katika Patakatifu Zaidi.

  • Siku ya Upatanisho (Atonement Day)
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Haruni alitoa yule fahali kuwa dhabihu kwa ajili ya makuhani na wale wengine wa kabila la Lawi, akinyunyiza damu yake katika Patakatifu Zaidi. (Law 16:11, 14) Kwa kulinganisha Kristo alitoa thamani ya damu yake ya kibinadamu kwa Mungu mbinguni, ambako ingeweza kutumiwa kufaidi wale ambao wangekuja kutawala pamoja naye wakiwa makuhani na wafalme. (Ufu 14:1-4; 20:6) Yule mbuzi kwa ajili ya Yehova alitolewa dhabihu pia na damu yake ilinyunyizwa mbele ya Sanduku la Agano katika Patakatifu Zaidi, jambo hilo likifanywa ili kufaidi yale makabila ya Israeli yasiyo ya kikuhani. (Law 16:15) Hali moja na hiyo, ile dhabihu moja ya Yesu Kristo hufaidi pia jamii ya wanadamu zaidi ya kufaidi Israeli wa kikuhani wa kiroho. Mbuzi wawili walihitajiwa, kwa maana mbuzi mmoja tu hangeweza kutumika akiwa dhabihu na bado atumiwe kuchukua dhambi za Israeli. Mbuzi wote wawili walitajwa kuwa toleo moja la dhambi. (Law 16:5) nao walitendewa kwa njia ileile moja hadi wakati wa kutupwa kwa kura juu yao, jambo ambalo linaonyesha kwamba wakiwa pamoja walifananisha kitu kimoja. Si kwamba tu Yesu Kristo alitolewa dhabihu bali pia alichukua dhambi za wale ambao alikufa kama dhabihu kwa ajili yao.

  • Azazeli
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Mbuzi wote wawili walikuwa kwa ajili ya dhabihu moja ya dhambi. (Law 16:5) Mbuzi wawili walitumiwa ili kukazia jambo lililotimizwa na uandalizi huo wa kufunika dhambi za watu. Mbuzi wa kwanza alitolewa dhabihu. Yule wa pili, alibeba dhambi za watu juu yake na akapelekwa nyikani, na hilo linaongeza uzito kwenye msamaha ambao Yehova huwapa wanaotubu. Zaburi 103:12 inatupatia uhakikisho huu: “Kama mashariki ilivyo mbali sana na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali sana na sisi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki