Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Upatanisho (Atonement Day)
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Haruni, akiwa anarudi kutoka Patakatifu Zaidi, alichukua sehemu ya damu ya yule fahali, na kuingia chumba hicho akiwa nayo, na kunyunyiza sehemu ya damu hiyo kwa kidole chake mara saba mbele ya kifuniko cha Sanduku la Agano katika upande wa Mashariki. Hivyo ndivyo upatanisho wa ukuhani ulivyokamilishwa, hilo likiwafanya makuhani wawe safi na kuweza kufanya upatanisho kati ya Yehova na watu wake.—Law 16:14.

  • Siku ya Upatanisho (Atonement Day)
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Haruni alitoa yule fahali kuwa dhabihu kwa ajili ya makuhani na wale wengine wa kabila la Lawi, akinyunyiza damu yake katika Patakatifu Zaidi. (Law 16:11, 14) Kwa kulinganisha Kristo alitoa thamani ya damu yake ya kibinadamu kwa Mungu mbinguni, ambako ingeweza kutumiwa kufaidi wale ambao wangekuja kutawala pamoja naye wakiwa makuhani na wafalme. (Ufu 14:1-4; 20:6) Yule mbuzi kwa ajili ya Yehova alitolewa dhabihu pia na damu yake ilinyunyizwa mbele ya Sanduku la Agano katika Patakatifu Zaidi, jambo hilo likifanywa ili kufaidi yale makabila ya Israeli yasiyo ya kikuhani. (Law 16:15) Hali moja na hiyo, ile dhabihu moja ya Yesu Kristo hufaidi pia jamii ya wanadamu zaidi ya kufaidi Israeli wa kikuhani wa kiroho. Mbuzi wawili walihitajiwa, kwa maana mbuzi mmoja tu hangeweza kutumika akiwa dhabihu na bado atumiwe kuchukua dhambi za Israeli. Mbuzi wote wawili walitajwa kuwa toleo moja la dhambi. (Law 16:5) nao walitendewa kwa njia ileile moja hadi wakati wa kutupwa kwa kura juu yao, jambo ambalo linaonyesha kwamba wakiwa pamoja walifananisha kitu kimoja. Si kwamba tu Yesu Kristo alitolewa dhabihu bali pia alichukua dhambi za wale ambao alikufa kama dhabihu kwa ajili yao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki