-
Jenga Itibari Katika Yehova kwa Kujifunza Neno Lake kwa Bidii-EndelevuMnara wa Mlinzi—1988 | Agosti 15
-
-
‘Kuelekeza Kabisa Mioyo Yao’ Kwenye Neno la Mungu
3, 4. (a) Waisraeli walipaswa ‘kuelekeza kabisa mioyo yao’ kwenye kitu gani, na hiyo ilihusisha nini ndani? (b) Vizazi vya baadaye vilitumia shauri la Musa jinsi gani?
3 Musa aliwaonya Waisraeli kwa upole ‘waelekeze kabisa mioyo yao’ si kwenye wimbo wake wenye kusisimua tu, bali kwenye miandiko yote mitakatifu. Ilikuwa lazima wao ‘wafanye usikizi mwema’ (Knox), ‘wawe na uhakika wa kutii’ (Today’s English Version), au ‘watafakari juu ya’ (The Living Bible) Sheria ya Mungu. Ni kwa kujifahamisha nayo sana sana tu kwamba wangeweza ‘kuamuru wana wao wafanye uangalifu kutenda maneno yote ya sheria hii.’ Kwenye Kumbukumbu 6:6-8, NW, Musa aliandika hivi: “Maneno haya ambayo mimi ninaamuru wewe leo ni lazima yathibitike kuwa juu ya moyo wako; na ni lazima wewe uyakaze kikiki katika mwana wako . . . Na ni lazima wewe uyafunge yakiwa ishara juu ya mkono wako, na ni lazima yatumike kuwa kifungio cha mbele kati ya macho yako.”
-
-
Jenga Itibari Katika Yehova kwa Kujifunza Neno Lake kwa Bidii-EndelevuMnara wa Mlinzi—1988 | Agosti 15
-
-
5. Ni nini uliokuwa utumizi unaofaa wa maneno ya Musa kwenye Kumbukumbu 6:6-8?
5 Sivyo, Sheria ya Mungu haikupasa kukaa juu ya mikono yao halisi wala vipaji vya nyuso halisi bali ‘juu ya mioyo yao.’ Kwa kupata si maarifa juu yayo tu bali pia uthamini wenye kina kirefu kwa maarifa hayo, ndipo Sheria hiyo ingewekwa ikionekana wazi, kama kwamba imeandikwa juu ya ubao mbele ya macho yao au imefungwa juu ya mikono yao.
-