Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Aliandalia Israeli Katika Sinai
    Mnara wa Mlinzi—1992 | Mei 1
    • EBU wazia mamilioni ya—wanaume, wanawake, na watoto—wakielekea kuingia “jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji”!

      Maneno hayo ya Mungu yanayopatikana kwenye Kumbukumbu la Torati 8:15 hukazia ile ambayo huenda ikaonekana kuwa safari yenye kuhofisha iliyokuwa mbele ya Waisraeli walipotoka Misri na kwenda kwa miguu ndani ya jangwa la Sinai. Tatizo moja kubwa: Nani angeandaa chakula na maji ya kutosha?

  • Aliandalia Israeli Katika Sinai
    Mnara wa Mlinzi—1992 | Mei 1
    • Baada ya Waisraeli kuvuka Bahari Nyekundu, walipata kuelewa jinsi Sinai ilivyokuwa hasa. Hawakufuata ile njia ya biashara iliyofuatwa kwa kawaida iliyokuwa upande wa kaskazini bali waligeuka kuelekea ukingo wa peninsula hiyo ya pembetatu. Kufikia wakati walipokuwa wameenda kilometa yapata 80 kupitia jangwa hilo, uhitaji wao wa maji ulionekana kuwa mkubwa. Wasingeweza kunywa maji yale waliyopata, kwa kuwa yalikuwa machungu na labda yalikuwa na magonjwa. “Tunywe nini?” wakalia. Mungu aliingilia, akigeuza maji hayo kuwa matamu.—Kutoka 15:22-25.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki