Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Alitangazwa Kuwa Mwadilifu kwa Matendo’
    Mnara wa Mlinzi—2013 | Novemba 1
    • RAHABU YULE KAHABA

      Rahabu alikuwa kahaba. Jambo hilo liliwashangaza sana wafafanuzi fulani wa Biblia hivi kwamba wakadai alifanya kazi katika nyumba ya wageni. Hata hivyo, Biblia inasema mambo waziwazi na haifichi ukweli. (Yoshua 2:1; Waebrania 11:31; Yakobo 2:25) Inawezekana kazi ya Rahabu iliheshimiwa na Wakanaani. Hata hivyo, utamaduni hauwezi kuzuia dhamiri kwa sababu Yehova aliwapa watu wote uwezo huo wa kutambua mema na mabaya. (Waroma 2:14, 15) Huenda Rahabu alitambua kwamba maadili yake yalikuwa mapotovu. Labda, kama wengi leo, alihisi amenaswa, bila njia nyingine ya kutunza familia yake.

  • ‘Alitangazwa Kuwa Mwadilifu kwa Matendo’
    Mnara wa Mlinzi—2013 | Novemba 1
    • ALIWAPOKEA WALE WAPELELEZI

      Siku moja, kabla ya Waisraeli kuzunguka jiji la Yeriko, wageni wawili walimtembelea Rahabu. Wanaume hao walifikiri hawangetambuliwa na mtu yoyote, lakini watu walikuwa na wasiwasi jijini na hivyo waliwatambua kwa urahisi wapelelezi hao Waisraeli. Huenda Rahabu aliwatambua mara moja. Hakushangaa alipotembelewa na wanaume wageni, lakini alishangaa kujua kwamba wanaume hao walitaka mahali pa kulala bali si huduma zake za ukahaba.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki