-
“Uendako Nitaenda”Igeni Imani Yao
-
-
18 Basi, wakaendelea na safari wakiwa wawili tu, kwenye barabara ndefu ya kwenda Bethlehemu. Inakadiriwa kwamba huenda safari hiyo ilichukua juma moja. Bila shaka, ingawa walikuwa na majonzi walifarijiana kwa kiasi fulani.
-
-
“Uendako Nitaenda”Igeni Imani Yao
-
-
21 Hatimaye, wanawake hao wawili waliwasili Bethlehemu, kijiji kilichokuwa karibu kilomita 10 upande wa kusini wa Yerusalemu. Inaonekana Naomi na familia yake walijulikana sana katika mji huo mdogo, kwa kuwa habari za kurudi kwake zilisambaa kila mahali. Wanawake katika eneo hilo walimtazama na kuulizana, “Je, huyu ni Naomi?” Bila shaka, alikuwa amebadilika baada ya kuishi Moabu; kwa kumtazama, watu waliona kwamba alikuwa amekabiliana na matatizo na majonzi kwa miaka mingi.—Rut. 1:19.
-