-
“Uendako Nitaenda”Mnara wa Mlinzi—2012 | Julai 1
-
-
Basi, wakaendelea na safari wakiwa wawili tu, kwenye barabara ndefu ya kwenda Bethlehemu. Kulingana na mkadiriaji mmoja, huenda safari hiyo ilichukua juma moja. Bila shaka, ingawa walikuwa na huzuni kila mmoja wao alifarijiwa na mwenzake kwa kiasi fulani.
-
-
“Uendako Nitaenda”Mnara wa Mlinzi—2012 | Julai 1
-
-
Hatimaye, wanawake hao wawili waliwasili Bethlehemu, kijiji kilichokuwa karibu kilomita 10 upande wa kusini wa Yerusalemu. Inaonekana Naomi na familia yake walijulikana sana katika mji huo mdogo, kwa kuwa habari kwamba alikuwa amerudi zilisambaa kila mahali. Wanawake katika eneo hilo walimtazama na kuulizana, “Je, huyu ni Naomi? ” Bila shaka, alikuwa amebadilika baada ya kutoka Moabu; kwa kutazama sura na umbo lake, watu wangeona kwamba alikuwa amekabiliana na matatizo na huzuni kwa miaka mingi.—Ruthu 1:19.
-