-
“Mwanamke Bora Sana”Igeni Imani Yao
-
-
1, 2. (a) Ruthu alikuwa akifanya kazi gani? (b) Ruthu alitambua mambo gani mazuri kuhusu Sheria ya Mungu na watu wake?
RUTHU alipiga magoti kando ya vishina vya shayiri ambavyo alikuwa amekusanya mchana. Giza lilikuwa likiingia kwenye mashamba huko Bethlehemu, na tayari wafanyakazi wengi walikuwa wakielekea kwenye lango la jiji dogo lililokuwa juu ya bonde ambalo lilikuwa karibu. Ruthu alihisi maumivu ya uchovu baada ya kufanya kazi mchana kutwa. Lakini, aliendelea kupiga vishina akitumia ufito mdogo au gongo ili apatenafaka. Ingawa hivyo, ilikuwa siku njema, kuliko jinsi alivyotazamia.
-
-
“Mwanamke Bora Sana”Igeni Imani Yao
-
-
5, 6. (a) Ruthu alifanikiwa kupata nini siku yake ya kwanza ya kukusanya masalio kwenye mashamba ya Boazi? (b) Naomi alitendaje alipomwona Ruthu?
5 Ruthu alipomaliza kupura nafaka na kuikusanya, alitambua kwamba alikuwa amekusanya shayiri karibu kipimo kimoja cha efa. Huenda mzigo wake ulikuwa na uzito wa kilo 14! Akainua mzigo wake, labda akiwa ameufunga kwa kitambaa na kuubeba kichwani, kisha akatembea kuelekea Bethlehemu huku jua likitua.—Rut. 2:17.
-