-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
Boazi aliendelea kusema: “Basi sasa, binti yangu, usiogope. Yote utakayosema nitakufanyia, kwa maana kila mtu aliye katika lango la watu wangu anajua kwamba wewe ni mwanamke bora sana.” (Ruthu 3:11) Alipendezwa na wazo la kumwoa Ruthu; labda hakushangaa alipoombwa kuwa mkombozi wake. Hata hivyo, Boazi alikuwa mwanamume mwadilifu na hakuwa tayari kutenda tu kulingana na mapendezi yake. Alimwambia Ruthu kwamba kulikuwa na mkombozi mwingine ambaye alikuwa mtu wa ukoo wa karibu zaidi wa mume wa Naomi aliyekuwa amekufa; Boazi angezungumza na mwanamume huyo kwanza na kumpa nafasi ya kuwa mume wa Ruthu.
-
-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
Kwa kweli Ruthu aliridhika sana alipotafakari mambo ambayo Boazi alikuwa amemwambia, kwamba alijulikana na watu wote kuwa “mwanamke bora sana”! Bila shaka, tamaa yake ya kutaka kumjua Yehova na kumtumikia ilimsaidia sana ajulikane kwa njia hiyo. Pia, alikuwa amemtendea Naomi na watu wake kwa fadhili na ufikirio sana, akifuata kwa hiari njia na desturi ambazo hakuzijua mwanzoni. Tukiiga imani ya Ruthu, tutajitahidi kuwaonyesha wengine heshima na kuheshimu njia na desturi zao. Tukifanya hivyo, sisi pia tunaweza kutambua kwamba tunajulikana kuwa watu bora sana.
-