-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1986 | Juni 1
-
-
Kiapo ambacho Sauli alifanya haraka-haraka kiliingiza Israeli katika uwezekano wa kupata laana, lakini haionekani kwamba Yonathani alistahili kupoteza upendeleo wa Yehova kwa sababu ya kutenda kinyume cha kiapo hicho.
Samweli wa Kwanza 14:24-45 inasimulia kisa hicho. Kwa kutiwa ujasiri na matendo hodari yaliyofanywa na Yonathani, Waisraeli walikuwa wakipigana na Wafilisti maadui. Mfalme Sauli alisema: “Na alaaniwe mtu awaye yote alaye chakula cho chote hata jioni, nipate kujilipiza kisasi juu ya adui zangu.” (mst. 24) Kwa kutojua kiapo kilichofanywa na Baba yake, Yonathani alijipatia nishati kwa kula kiasi fulani cha asali. Mashujaa wengine Waisraeli, waliokuwa pia wameishiwa na nguvu, walitenda dhambi kwa kuchinja ng’ombe na kula kwa pupa nyama isiyokaushwa damu vizuri. Sauli alijenga madhabahu kuhusu dhambi hiyo, lakini hakujua alilokuwa amefanya mwanaye.
Sauli alipotafuta mwelekezo wa Mungu ili asukume pigano mbele, Yehova hakujibu. Kwa kutumia Thumimu (labda iliotia ndani kura takatifu za kutupwa), Sauli alipata habari kwamba mwanaye alikuwa amekivunja kile kiapo kilichotolewa kwa njia isichofaa. Lakini je, kwa kweli Yonathani alikuwa na hatia?
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1986 | Juni 1
-
-
Mungu aliruhusu matumizi ya Thumimu ili ijulikana kwamba Yonathani alikuwa amevunja (bila kujua) kiapo cha Sauli, lakini hiyo haimaanisha kwamba Yeye alikikubali kiapo hicho kwa haraka-haraka. Masimulizi hayasemi po pote kwamba Mungu alimwona Yonathani kuwa mwenye kustahili adabu. Kwa kweli, ingawa Yonathani alikuwa na nia ya kukubali matokeo ya kuvunja kiapo cha babaye kilichofanywa kwa haraka, hali zilienda kwa njia ambayo uhai wa Yonathani uliachiliwa. Askari Waisraeli walisema kwamba Yonathani alikuwa amefanya matendo hodari “na Mungu,” na kwa njia fulani wakamkomboa Yonathani. Katika miaka iliyofuata, Yonathani ndiye aliyeendelea kuwa na kibali cha Yehova huku Sauli akizidi kutenda kosa moja baada ya jingine.
-