-
Mtu Anayekubalika kwa Moyo wa YehovaMnara wa Mlinzi—2011 | Septemba 1
-
-
Daudi alikabili hatari mbalimbali akiwa mchungaji. Ni katika milima hiyo ambapo Daudi alipambana na simba na dubu waliojaribu kuchukua kondoo aliokuwa akichunga.a Kijana huyo mjasiri aliwakimbiza wanyama hao wawindaji, akawaua, na kuwaokoa kondoo wake kutoka midomoni mwao. (1 Samweli 17:34-36) Huenda ni wakati huo ambapo Daudi alipata ustadi wa kutumia kombeo. Eneo la kabila la Benyamini lilikuwa karibu na mji wao. Walenga shabaha wa kabila hilo walitupa mawe kwa kombeo na wangeweza “kupiga shabaha unywele, bila kukosea.” Daudi pia alikuwa na ustadi kama huo wa kutumia kombeo.—Waamuzi 20:14-16; 1 Samweli 17:49.
-
-
Mtu Anayekubalika kwa Moyo wa YehovaMnara wa Mlinzi—2011 | Septemba 1
-
-
a Dubu wa rangi ya kahawia wa Siria waliopatikana katika eneo la Palestina, walikuwa na uzito wa kilo 140 hivi na walikuwa na uwezo wa kuua mnyama au mwanadamu kwa kumpiga kwa miguu yao mikubwa ya mbele. Wakati fulani kulikuwa na simba wengi katika eneo hilo. Andiko la Isaya 31:4 linasema kuwa hata “hesabu kamili ya wachungaji” hawangeweza kumfukuza “mwana-simba mwenye manyoya shingoni” kutoka kwa windo lake.
-