-
“Kile Unachoweka Nadhiri, Timiza”Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2017 | Aprili
-
-
7. (a) Hana alitoa nadhiri gani, na kwa nini, na matokeo yalikuwa nini? (b) Nadhiri ya Hana ilibadili maisha ya Samweli jinsi gani? (Tazama maelezo ya chini.)
7 Mfano mwingine ni Hana, ambaye alitimiza kwa uaminifu nadhiri aliyomwekea Yehova. Alitoa ahadi yake akiwa amefadhaika na akiwa na mkazo mwingi kwa kuwa alikuwa tasa na alidhihakiwa sana. (1 Sam. 1:4-7, 10, 16) Hana alimmiminia Mungu moyo wake na kutoa nadhiri hii: “Ee Yehova wa majeshi, ikiwa hakika utayaona mateso ya kijakazi wako, nawe kwa kweli unikumbuke, na ikiwa hutamsahau kijakazi wako na kwa kweli umpe kijakazi wako uzao wa kiume, mimi nitamtoa kwa Yehova siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita juu ya kichwa chake.”a (1 Sam. 1:11) Ombi la Hana lilijibiwa, naye akamzaa mwana, mzaliwa wa kwanza. Alifurahi sana! Lakini hakusahau nadhiri aliyokuwa ameweka kwa Mungu. Alipomzaa mwanawe, alitangaza hivi: “Nimemwomba kutoka kwa Yehova.”—1 Sam. 1:20.
-