-
Alitenda kwa BusaraMnara wa Mlinzi—2009 | Julai 1
-
-
Nabali aliishi huko Maoni lakini alifanya kazi katika mji wa karibu wa Karmeli ambako inaelekea alikuwa na shamba.a Miji hiyo miwili ilikuwa na maeneo yaliyoinuka yenye nyasi yaliyofaa kwa ufugaji wa kondoo, ambako Nabali alikuwa na kondoo 3,000. Hata hivyo, maeneo yote ya kandokando yalikuwa mbuga. Kulikuwa na jangwa kubwa la Parani upande wa kusini. Upande wa mashariki, kulikuwa na barabara iliyoelekea kwenye Bahari ya Chumvi iliyopitia maeneo makavu yenye mabonde na mapango. Daudi na wanaume wake walifanya yote waliyoweza ili kuishi katika maeneo hayo. Bila shaka, waliwinda wanyama ili kupata chakula huku wakivumilia hali nyingi ngumu. Walikutana mara nyingi na vijana wachungaji ambao walimtumikia tajiri Nabali.
-
-
Alitenda kwa BusaraMnara wa Mlinzi—2009 | Julai 1
-
-
a Huo haukuwa ule Mlima Karmeli unaojulikana ulio mbali huko kaskazini, bali ni mji ulio kwenye ukingo wa jangwa la kusini.
-