-
Alitenda kwa BusaraIgeni Imani Yao
-
-
10 Askari-jeshi hao wenye bidii waliwatendeaje wale wachungaji? Ingekuwa rahisi kwao kuchukua kondoo mara kwa mara, lakini hawakufanya hivyo. Badala yake, walilinda mifugo ya Nabali na watumishi wake. (Soma 1 Samweli 25:15, 16.) Kondoo na wachungaji walikabili hatari nyingi. Kulikuwa na wanyama wengi hatari, na mpaka wa kusini wa Israeli ulikuwa karibu sana hivi kwamba wezi na waporaji wa nchi nyingine walivamia mara kwa mara.b
-
-
Alitenda kwa BusaraIgeni Imani Yao
-
-
b Inaelekea Daudi alihisi kwamba kuwalinda wakulima Waisraeli na mifugo yao kulikuwa utumishi kwa Yehova Mungu. Siku hizo, Yehova alikusudia kwamba wazao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo waishi katika nchi hiyo. Hivyo, kuilinda nchi hiyo isivamiwe na vikundi vya waporaji wa kigeni kulikuwa utumishi mtakatifu.
-