-
Alimweleza Mungu Mahangaiko YakeIgeni Imani Yao
-
-
9. Tunajifunza nini kutokana na utayari wa Hana wa kusafiri kwenda Shilo ingawa alijua jinsi ambavyo Penina angemtendea?
9 Asubuhi na mapema, familia nzima ilikuwa na pilikapilika nyingi. Kila mtu alikuwa akijitayarisha kwa safari, kutia ndani watoto. Safari hiyo ya kwenda Shilo ilikuwa ya kilomita zaidi ya 30 kuvuka nchi ya Efraimu yenye milima-milima.b Safari hiyo ingechukua siku moja au mbili kwa miguu. Hana alijua jinsi ambavyo Penina angemtendea. Hata hivyo, hakubaki nyumbani. Kwa hiyo, akawawekea mfano mzuri waabudu wa Mungu mpaka leo. Si jambo la hekima kuruhusu mwenendo mbaya wa wengine utuzuie kumwabudu Mungu. Tukiruhusu watuzuie, tutakosa baraka zinazotusaidia kuvumilia.
-
-
Alimweleza Mungu Mahangaiko YakeIgeni Imani Yao
-
-
b Umbali huo unategemea uwezekano wa kwamba mji wa nyumbani wa Elkana ulikuwa Rama, eneo ambalo baadaye katika siku za Yesu liliitwa Arimathea.
-