-
Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia SalaMnara wa Mlinzi—2010 | Julai 1
-
-
HANA alikuwa akijitayarisha kwa ajili ya safari, huku akijaribu kusahau matatizo yake. Hiyo ilipaswa kuwa pindi yenye furaha; kila mwaka, Elkana, mume wake alikuwa na desturi ya kusafiri na familia yake yote kuelekea kwenye maskani huko Shilo. Yehova alitaka pindi hizo ziwe zenye shangwe. (Kumbukumbu la Torati 16:15) Na bila shaka tangu utotoni Hana alikuwa amefurahia sherehe hizo. Lakini mambo yalikuwa yamebadilika katika miaka ya hivi karibuni.
-
-
Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia SalaMnara wa Mlinzi—2010 | Julai 1
-
-
Asubuhi na mapema, familia nzima ilikuwa na pilikapilika nyingi. Kila mtu alikuwa akijitayarisha kwa ajili ya safari, kutia ndani watoto. Safari hiyo ya kwenda Shilo ilikuwa ya kilomita 30 kuvuka nchi ya Efraimu yenye milima-milima.c Safari hiyo ingechukua siku moja au mbili kwa miguu. Hana alijua jinsi mke mwenzake angemtendea. Hata hivyo, Hana hakubaki nyumbani. Hivyo anawawekea waabudu wa Mungu leo mfano mzuri. Si jambo la hekima kuruhusu mwenendo wa wengine utuzuie tusimwabudu Mungu. Ikiwa tutafanya hivyo tutakosa baraka zitakazotuwezesha kuvumilia.
-
-
Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia SalaMnara wa Mlinzi—2010 | Julai 1
-
-
c Huenda umbali huo ulikadiriwa hivyo kwa sababu mji wa Rama ambako Elkana aliishi ni mji uliokuja kuitwa Arimathea katika siku za Yesu.
-