Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kuna Thawabu kwa Ajili ya Kazi Yenu”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • Aliporudi kutoka vitani, Asa alikutana na Azaria. Nabii huyo alimtia moyo na kumwonya pia: “Mnisikilize mimi, Ee Asa na Yuda wote na Benyamini! Yehova yuko pamoja nanyi ikiwa ninyi mko pamoja naye; nanyi mkimtafuta, atawaruhusu mumpate, lakini mkimwacha yeye atawaacha ninyi. . . . Iweni hodari na msiache mikono yenu ilegee, kwa sababu kuna thawabu kwa ajili ya kazi yenu.”​—2 Nya. 15:1, 2, 7.

      Maneno hayo yanaweza kuimarisha imani yetu. Yanaonyesha kwamba Yehova atakuwa pamoja nasi maadamu tunamtumikia kwa uaminifu. Tunapomlilia ili atusaidie, tunaweza kuwa na hakika kwamba anatusikiliza. Azaria alisema hivi: “Iweni hodari.” Kwa kawaida, uhodari mkubwa unahitajiwa ili kufanya mambo yanayofaa, lakini tunajua kwamba tunaweza kufanikiwa kwa msaada wa Yehova.

  • “Kuna Thawabu kwa Ajili ya Kazi Yenu”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • Hata hivyo, nabii Azaria alitoa pia onyo. Alionya hivi: “Mkimwacha [Yehova] atawaacha ninyi.” Isiwe hivyo kwetu kamwe, kwa kuwa matokeo yanaweza kuwa mabaya sana! (2 Pet. 2:20-22) Maandiko hayasemi kwa nini Yehova alimpa Asa onyo hilo, lakini mfalme huyo hakulitii.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki