-
MmetakaswaMnara wa Mlinzi—2013 | Agosti 15
-
-
Nehemia alionyeshaje ushikamanifu wake kwa Yehova? (Tazama fungu la 5 na 6)
5, 6. Eliashibu na Tobia walikuwa nani, na huenda ni kwa nini Eliashibu alishirikiana na Tobia?
5 Soma Nehemia 13:4-9. Tumezungukwa na uvutano usio safi, hivyo si rahisi kwetu kuendelea kuwa watakatifu. Mfikirie Eliashibu na Tobia. Eliashibu alikuwa kuhani mkuu, na inaelekea kwamba Tobia alikuwa Mwamoni na ofisa wa cheo cha chini katika utawala wa Uajemi huko Yudea. Tobia na wenzake walipinga jitihada za Nehemia za kujenga upya kuta za Yerusalemu. (Neh. 2:10) Waamoni hawakuruhusiwa kuingia katika uwanja wa hekalu. (Kum. 23:3) Basi, kwa nini kuhani mkuu alimruhusu Tobia akae katika jumba la kulia chakula la hekalu?
6 Tobia alikuwa rafiki wa karibu wa Eliashibu. Tobia na Yehohanani, mwana wake, walioa wanawake Wayahudi, na Wayahudi wengi walimsifu sana Tobia. (Neh. 6:17-19) Mmoja wa wajukuu wa Eliashibu alimwoa binti ya Sanbalati, gavana wa Samaria aliyekuwa mmoja wa rafiki wa karibu sana wa Tobia. (Neh. 13:28) Mahusiano hayo yanaweza kutusaidia kuelewa ni kwa nini Kuhani Mkuu Eliashibu aliruhusu mtu asiye mwamini na aliye mpinzani amwongoze vibaya. Hata hivyo, Nehemia alionyesha ushikamanifu kwa Yehova kwa kutupa fanicha za Tobia nje ya jumba la kulia chakula.
-
-
MmetakaswaMnara wa Mlinzi—2013 | Agosti 15
-
-
8. Watumishi wote wa Yehova waliojiweka wakfu wanapaswa kukumbuka nini kuhusu watu wanaoshirikiana nao?
8 Tunapaswa kukumbuka kwamba “mashirika mabaya huharibu tabia nzuri.” (1 Kor. 15:33) Huenda baadhi ya watu wetu wa ukoo wakawa mashirika mabaya. Eliashibu aliwawekea wengine mfano mzuri kwa kumuunga mkono kikamili Nehemia katika kujenga upya kuta za Yerusalemu. (Neh. 3:1) Hata hivyo, inaonekana kwamba uvutano mbaya wa Tobia na watu wengine ulimchochea Eliashibu kufanya mambo yaliyomfanya kuwa mchafu mbele za Yehova. Mashirika mazuri hututia moyo kufuatilia mambo ya Kikristo yenye kujenga kama vile kusoma Biblia, kuhudhuria mikutano ya Kikristo, na kushiriki katika utumishi wa shambani. Tunawapenda na kuwathamini sana washiriki wa familia wanaotuchochea kufanya yaliyo sawa.
-