Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Aliwatetea Watu wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
    • Mwanamume aliyeitwa Hamani alipewa cheo cha juu katika utawala wa Ahasuero. Mfalme alimchagua Hamani kuwa waziri mkuu, hivyo akawa mshauri wake mkuu na mtu wa pili kwa cheo katika milki yake. Hata mfalme aliagiza kwamba kila mtu amwinamie anapomwona. (Esta 3:1-4) Sheria hiyo ilitokeza tatizo kubwa kwa Mordekai. Alijua kwamba alipaswa kumtii mfalme, lakini hangefanya hivyo ikiwa jambo hilo lingemvunjia Mungu heshima. Ona kwamba Hamani alikuwa “Mwagagi.” Hilo linamaanisha kwamba alikuwa mzao wa Agagi, mfalme wa Waamaleki ambaye aliuawa na Samweli, nabii wa Mungu. (1 Samweli 15:33) Waamaleki walikuwa waovu sana na hivyo wakawa maadui wa Yehova na Waisraeli. Taifa la Waamaleki lilihukumiwa na Mungu.b (Kumbukumbu la Torati 25:19) Myahudi mwaminifu angewezaje kumwinamia Mwamaleki mwenye mamlaka? Mordekai hangefanya hivyo. Alisimama imara. Leo pia, wanaume na wanawake wenye imani wamehatarisha maisha yao kwa kutii kanuni hii: “Lazima tumtii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.”—Matendo 5:29.

  • Aliwatetea Watu wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
    • b Yaelekea Hamani alikuwa mmoja wa wazao wa mwisho-mwisho wa Waamaleki, kwa sababu wale ‘waliobaki’ waliangamizwa katika siku za Mfalme Hezekia.—1 Mambo ya Nyakati 4:43.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki