-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
18. (a) Kwa nini Mordekai alikataa kumwinamia Hamani? (Ona pia maelezo ya chini.) (b) Leo, wanaume na wanawake wenye imani wanaigaje mfano wa Mordekai?
18 Mwanamume anayeitwa Hamani alipandishwa cheo katika makao ya Ahasuero. Mfalme alimchagua Hamani kuwa waziri mkuu, na akawa mshauri wake mkuu na mtu wa pili kwa cheo katika milki yake. Hata mfalme aliagiza kwamba kila mtu amwinamie anapomwona. (Esta 3:1-4) Sheria hiyo ilimsababishia Mordekai matatizo. Alipaswa kumtii mfalme, lakini hangefanya hivyo ikiwa jambo hilo lingemvunjia Mungu heshima. Hamani alikuwa Mwagagi. Hilo linamaanisha kwamba alikuwa mzao wa Agagi, mfalme wa Waamaleki ambaye aliuawa na Samweli, nabii wa Mungu. (1 Sam. 15:33) Waamaleki walikuwa waovu sana na hivyo wakawa maadui wa Yehova na Waisraeli. Waamaleki walikuwa na hatia mbele za Mungu.c (Kum. 25:19) Myahudi mwaminifu angewezaje kumwinamia Mwamaleki? Mordekai hakufanya hivyo. Alisimama imara. Leo pia, wanaume na wanawake wenye imani wamehatarisha uhai wao kwa kutii kanuni hii: “Lazima tumtii Mungu kuwa mtawala kuliko wanadamu.”—Mdo. 5:29.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
c Huenda Hamani alikuwa mmoja wa wazao wa mwisho-mwisho wa Waamaleki, kwa sababu wale ‘waliobaki’ walikuwa wameangamizwa katika siku za Mfalme Hezekia.—1 Nya. 4:43.
-