-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1991 | Februari 15
-
-
Ilipoonekana kwamba Ayubu angeweza kufa, Elihu alikadiria hali yake hatari na kuuweka msingi kwa ajili ya tumaini, akisema hivi: “Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane . . . Na uhai wake unakaribia waangamizi. Kwamba akiwapo malaika [mjumbe, NW] pamoja naye, mkalimani [mnenaji, NW], mmoja katika elfu, ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo; ndipo amwoneapo rehema, na kusema, mwokoe asishuke shimoni; mimi nimeuona ukombozi. Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto.”—Ayubu 33:21-25.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1991 | Februari 15
-
-
Ilitendeka hivyo. Ayubu ‘alitubu katika mavumbi na majivu.’ Halafu? “BWANA [Yehova, NW] akaugeuza uteka wa Ayubu . . . Basi hivyo BWANA [Yehova, NW] akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake . . . Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne.” Yakubalika kwamba ukombozi huo haukumweka Ayubu huru kutoka dhambi, hivyo basi baada ya muda alikufa. Hata hivyo, kurefushwa kwa uhai wake kwathibitisha kwamba, kwa matokeo ya kustaajabisha, ‘nyama ya mwili wake ilipata kuwa laini kuliko ya mtoto, akazirudia siku za ujana wake.’—Ayubu 33:25; 42:6, 10-17.
-