-
“Waangalieni kwa Makini Ndege”Amkeni!—2014 | Agosti
-
-
Mara nyingi Biblia huwataja ndege ili kutufundisha masomo muhimu. Kwa mfano, kuhusu mwendo-kasi wa mbuni, Mungu alimwambia Ayubu hivi: “Wakati anapopiga-piga mabawa yake juu, yeye humcheka farasi na mpandaji wake.”a (Ayubu 39:13, 18) Pia, Mungu alimuuliza Ayubu: “Je, ni kwa sababu ya uelewaji wako kwamba kipanga hupaa juu, . . . au, je, ni kwa agizo lako kwamba tai huruka kuelekea juu?” (Ayubu 39:26, 27) Tunajifunza nini? Ndege wanafanya mambo makubwa bila msaada wetu. Uwezo wao unaonyesha hekima ya Mungu, bali si yetu.
-
-
“Waangalieni kwa Makini Ndege”Amkeni!—2014 | Agosti
-
-
a Mbuni ndiye ndege mkubwa zaidi, na hukimbia kwa kasi sana, akiwa na uwezo wa kukimbia kilomita 72 hivi kwa saa.
-