Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Utaitamani Sana”
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
    • Fikiria hali ilivyokuwa. Ayubu, mtu mwenye imani ya kipekee, anapatwa na majaribu makali. Anapoteza mali yake, anafiwa na watoto wake wote wapendwa, na anapatwa na ugonjwa mbaya. Akiwa katika maumivu makali anamlilia Mungu: “Laiti ungenificha katika Kaburi!” (Mstari wa 13) Ayubu anaona kuwa kaburini ni mahali anapoweza kupata kitulizo. Akiwa huko, atakuwa kama hazina ambayo Mungu ameificha na hatapatwa na matatizo wala maumivu.a

      Je, Ayubu atakaa kaburini milele? Ayubu anaamini kuwa haitakuwa hivyo. Anaendelea kusali: “Laiti . . . ungeniwekea kikomo cha wakati na kunikumbuka!” Ayubu anatumaini kwa uhakika kuwa hatakaa kaburini kwa muda mrefu na kwamba Yehova hatamsahau. Ayubu analinganisha wakati atakaokuwa kaburini na “kazi ya kulazimishwa”—kipindi ambacho atalazimika kungoja. Atangoja kwa muda gani? “Mpaka kitulizo changu kije,” anasema. (Mstari wa 14) Kitulizo hicho kitamaanisha kuwa atatoka kaburini—yaani, atafufuliwa!

  • “Utaitamani Sana”
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
    • a Kitabu kimoja cha marejeo kinasema kuwa neno hili la Ayubu, “ungenificha,” linaweza kumaanisha “u[ni]weke mahali salama kama akiba yenye thamani.” Kitabu kingine kinasema kwamba neno hilo linamaanisha “nifiche kama hazina.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki