Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tamati Inayokuja ya “Kitabu cha Vita vya Yehova”
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Julai 1
    • 12. Melkizedeki alikuwa picha ya Ofisa gani mkubwa zaidi wa Mungu Aliye Juu Zaidi, na ni zaburi gani iliyotungwa na Daudi humsema mmoja huyu kuwa kuhani na shujaa wa vita?

      12 Baada ya Abrahamu kushinda Kedorlaoma na wafalme washirika wake, Melkizedeki alimbariki. Melkizedeki Mfalme-Kuhani alikuwa picha ya kiunabii ya Mmoja ambaye angekuwa Kuhani wa Juu wa Mungu Aliye Juu Zaidi na pia shujaa wa vita mwenye uweza akiungwa mkono na Mungu Mkuu Kabisa. Mmoja huyu aliye mkubwa kuliko Melkizedeki wa Salemu ndiye huambiwa maneno ya Zaburi 110 iliyotungwa na Daudi mfalme aliye shujaa wa vita akiwa chini ya uvuvio, ambapo husema hivi: “BWANA [Yehova, NW] atainyosha toka Sayuni fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako . . . BWANA [Yehova, NW] ameapa, wala hataghairi, ndiwe kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkizedeki. Bwana [Yehova, NW] yu mkono wako wa kuume; ataseta wafalme, siku ya ghadhabu yake.”—Zaburi 110:2, 4, 5.

      13. Katika Waebrania sura 7 na 8, Mmoja aliye mkubwa kuliko Melkizedeki wa zamani hutambulishwa kuwa nani, na Mmoja huyu aliingia katika mahali gani palipotukuka na akiwa na dhabihu ya aina gani?

      13 Mwandikaji aliyevuviwa wa kitabu cha Waebrania alifunua utambulisho wa yule Mmoja ambaye kwa kweli ndiye aliyeambiwa maneno hayo, aliposema hivi: “Mtangulizi ameingia kwa ajili yetu, Yesu, ambaye amekuwa kuhani wa juu kulingana na namna ya Melkizedeki milele.” (Waebrania 6:20, NW) Katika sura inayofuata ya Waebrania, uku-bwa wa Melkizedeki wa zamani waelezwa. Hata hivyo, ukubwa wake wa kikuhani ulipitwa na Mmoja ambaye yeye alitangulia kuwa kivuli cha ufananisho wake, yule Yesu Kristo aliyefufuliwa akatukuzwa, ambaye aliingia ndani ya kuwapo kutakatifu kwa Yehova Mungu mwenyewe akiwa na thamani ya dhabihu iliyo tukufu kuliko chochote ambacho Mfalme-Kuhani Melkizedeki wa Salemu angaliweza kutoa wakati wowote.—Waebrania 7:1–8:2.

  • Tamati Inayokuja ya “Kitabu cha Vita vya Yehova”
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Julai 1
    • 16 Nabii Isaya arejezea ubora wa jina hilo amtajapo Yehova kuwa “yule Mmoja anayefanya mkono Wake wenye upendezi uende kwenye kiganja cha kulia cha Musa; yule Mmoja anayegawanya maji kutoka mbele yao ili kufanya jina linalodumu kwa wakati usio dhahiri kwa ajili ya unafsi wake mwenyewe.” Naye akimwambia Yehova, asema hivi: “Hivyo wewe uliongoza watu wako ili ufanye jina lenye upendezi kwa ajili ya unafsi wako mwenyewe.” (Isaya 63:12-14, NW) Akimsihi Yehova atende tena kwa ajili ya watu wake, Danieli alisema naye kwa kumtaja kuwa “uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo.”—Danieli 9:15; Yeremia 32:20.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki