Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuyafuata Kwa Uangalifu Maagizo ya Mfalme
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Juni 1
    • “Nijishughulisha na maagizo yako, na mimi nitaangalia vijia vyako. Kwa sheria zako mimi nitaonyesha kutamani sana. Mimi sitasahau neno lako.”—ZABURI 119:15, 16,NW.

      1. Kwa sababu gani kila mtu na kila kitu kiko chini ya maagizo ya Yehova?

      KILA mtu na kila kitu kiko chini ya maagizo ya Mungu Mwenye Nguvu Zote Yehova, yule Mfalme wa umilele. Yeye ndiye aliyeumba ulimwengu mzima. Yeye ndiye Chanzo cha uhai wote. Yeye ndiye aliyeifanyiza dunia na kuitayarisha ikaliwe. Yeye ni Mungu wa utaratibu, na kwa kufililiza sheria zake, utaratibu utadumishwa katika sehemu zote za uumbaji wake.—Zaburi 36:9: Isaya 45:18; Ufunuo 15:3.

  • Kuyafuata Kwa Uangalifu Maagizo ya Mfalme
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Juni 1
    • 4. Watu wana mambo gani ya kuchagua, na matokeo ni nini?

      4 Lakini watu ni tofauti. Sisi tumeumbwa kwa sura ya Mungu, nasi tunaweza kujifanyia uchaguzi. Lakini, ingawa Yehova hakuingiza ndani yetu mipango ya kututendesha kwa hekima kwa kutegemea silika tu, wala yeye hakutuacha bila kujua la kufanya. Kupitia Neno lake Biblia, yeye anatupa sisi maagizo yake ya kupatia uzima. Tukiyafuata kwa uangalifu maagizo haya ya Mfalme, tutaishi. Tukitumia uhuru wetu kuyapuuza na kufuata barabara ya kujitegemea wenyewe, tutakufa. Ni lazima sisi tujipange wenyewe kwa njia itakayotuwezesha kuendeleza, uhai. Ni hivyo tu, hakuna zaidi. “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu,” akasema mtunga zaburi. Kwa upande mwingine, “barabara [tofauti] huenda ikaonekana kama kwamba ni nyofu kwa mtu, hata hivyo huenda ikaja kuwa ndiyo njia ya kifo.” (Zaburi 119:105; Mithali 14:12, The New English Bible) Katika wakati huu wa mwisho, ni lazima tujihusishe wenyewe na maneno ya Zaburi 119:15, 16, ambayo Yehova anaambiwa: “Nitayatafakari mausia [maagizo, NW ] yako, nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, sitalisahau neno lako.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki