-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
4. Kwa maneno yako mwenyewe, ungeelezaje yale yanayosemwa na Zaburi 133 kuhusu muungano wa kidugu?
4 Mtunga-zaburi Daudi alithamini sana muungano wa kidugu. Hata alipuliziwa kuimba juu yao! Ebu mwazie akiwa na kinubi chake huku akiimba: “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja [“muungano,” NW]. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Heremoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, naam, uzima hata milele.”—Zaburi 133:1-3.
-
-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
6, 7. Muungano wa Israeli ulikuwaje kama umande wa Mlima Heremoni, na baraka za Mungu zaweza kupatikana wapi leo?
6 Kukaa pamoja kwa Israeli kwa muungano kulikuwaje pia kama umande wa Mlima Heremoni? Kwa kuwa kilele cha mlima huo ni zaidi ya meta 2,800 juu ya usawa wa bahari, kina theluji karibu mwaka mzima. Kilele cha Heremoni chenye theluji husababisha utoneshaji wa mivuke ya usiku na hivyo hutokeza umande mwingi unaohifadhi mimea wakati wa ule msimu mkavu ulio mrefu. Mikondo ya hewa baridi kutoka safu ya milima ya Heremoni yaweza kuichukua mivuke hiyo kuelekea kusini hadi kufikia eneo la Yerusalemu, ambako inatoneka kuwa umande. Kwa hiyo mtunga-zaburi alisema kwa usahihi juu ya ‘umande wa Heremoni ukishuka juu ya Mlima Sayuni.’ Ni kikumbusha kizuri kama nini cha ule uvutano wenye kuburudisha unaoendeleza muungano wa familia ya waabudu wa Yehova!
7 Kabla ya kutaniko la Kikristo kuanzishwa, Sayuni, au Yerusalemu, lilikuwa kitovu cha ibada ya kweli. Basi, hapo ndipo mahali ambapo Mungu aliamuru baraka iwepo. Kwa kuwa Chanzo cha baraka zote kilikaa hekaluni Yerusalemu, baraka zingetoka huko kwa njia ya ufananisho. Basi, kwa sababu ibada ya kweli haitegemei tena mahali popote pamoja, baraka, upendo, na muungano wa watumishi wa Mungu zaweza kupatikana kotekote duniani leo. (Yohana 13:34, 35) Ni baadhi ya mambo gani yanayoendeleza muungano huu?
-