Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uumbaji Hutangaza Utukufu wa Mungu!
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Juni 1
    • 7 Hata hivyo, inahitaji utambuzi ili kusikia ushahidi huo. “Hakuna usemi, wala hakuna maneno; sauti yao haisikiki.” Hata hivyo, ushuhuda wa kimya-kimya wa mbingu una nguvu sana. “Kamba yake ya kupimia imefika duniani pote, na maneno yake yamefika kwenye miisho ya nchi yenye kuzaa.” (Zaburi 19:3, 4) Ni kana kwamba ‘kamba za kupimia’ kutoka mbinguni zimefika ili kuhakikisha kwamba ushahidi wao wa kimya-kimya umeenea kila mahali duniani.

      8, 9. Ni mambo gani yenye kutokeza kuhusu jua?

      8 Kisha, Daudi anaeleza jambo lingine lenye kustaajabisha kuhusu uumbaji wa Yehova: “Katika hizo [mbingu zinazoonekana] amewekea jua hema, nalo ni kama bwana-arusi anapotoka katika chumba chake cha ndoa; linashangilia kama mwanamume mwenye nguvu anapokimbia njiani. Linaenda kutoka mwisho mmoja wa mbingu, nao mzunguko wake humalizikia katika ile miisho yake mingine; wala hakuna chochote kilichofichwa kisiweze kupatwa na joto lake.”—Zaburi 19:4-6.

  • Uumbaji Hutangaza Utukufu wa Mungu!
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Juni 1
    • 10. (a) Jua huingiaje na kutoka katika “hema” lake? (b) Hukimbiaje kama “mwanamume mwenye nguvu”?

      10 Mtunga-zaburi anazungumza kuhusu jua kwa njia ya mfano, akilitaja kuwa “mwanamume mwenye nguvu” ambaye mchana hukimbia kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho ule mwingine na kupumzika usiku katika “hema.” Inapotazamwa kutoka duniani wakati wa kutua, nyota hiyo yenye nguvu huonekana kama inaingia katika “hema” kupumzika. Asubuhi huonekana kama linachomoka ghafula, likiangaza “kama bwana-arusi anapotoka katika chumba chake cha ndoa.” Akiwa mchungaji, Daudi alihisi baridi kali ya usiku. (Mwanzo 31:40) Alikumbuka jinsi yeye na eneo alimokuwa lilivyopashwa joto kwa haraka na miali ya jua. Ni wazi kwamba jua halikuwa limechoshwa na “safari” yake kutoka mashariki hadi magharibi lakini lilikuwa kama “mwanamume mwenye nguvu,” aliye tayari kuirudia safari yake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki