Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ifanye Mikono Ya Milele ya Yehova Iwe Utegemezo Wako
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Oktoba 1
    • 15. Ni nini maana ya maneno ya Daudi kwenye Zaburi 19:7-13?

      15 Ijapokuwa tunapenda sheria ya Yehova, nyakati nyingine tunakosa. Bila shaka hilo latutaabisha, kama lilivyomtaabisha Daudi, ambaye kwake sheria, makumbusho, amri, na maamuzi ya kihukumu ya Mungu vilikuwa vyenye kutamanika kuliko dhahabu. Alisema hivi: “Mtumishi wako huonywa kwazo, katika kuzishika kuna thawabu nyingi. Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi [vitendo vya kimbelembele, NW], yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.” (Zaburi 19:7-13) Acheni tuyachanganue maneno hayo.

  • Ifanye Mikono Ya Milele ya Yehova Iwe Utegemezo Wako
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Oktoba 1
    • 17. Dhambi zilizofichwa zaweza kuathirije mtu, hata hivyo, msamaha na kitulizo vyaweza kupatikanaje?

      17 Dhambi zilizofichwa zaweza kusababisha taabu. Kulingana na Zaburi 32:1-5, Daudi alijaribu kuficha dhambi yake, lakini alisema hivi: “Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa. Kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi.” Kujaribu kutuliza dhamiri yenye hatia kulimchokesha Daudi, na maumivu makali yalipunguza nguvu yake kama mti unavyopoteza umajimaji wenye kutoa uhai wakati wa ukame au katika joto kavu ya kaskazi. Yaonekana aliathiriwa vibaya kiakili na kimwili na kupoteza shangwe kwa sababu ya kukosa kuungama. Ungamo kwa Mungu ndio tu lingeweza kuleta msamaha na kitulizo. Daudi alisema hivi: “Heri [Mwenye furaha, NW] aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. . . . Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA [Yehova, NW]. Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.” Msaada wenye upendo kutoka kwa wazee Wakristo waweza kusaidia kuendeleza hali ya kupata nafuu kiroho.—Mithali 28:13; Yakobo 5:13-20.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki