Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova—Mungu Aliye Hodari kwa Nguvu Zake
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
    • 5. Tunapata ushuhuda gani wa nguvu za Yehova katika matendo yake?

      5 ‘Tukiyafikiria matendo ya Mungu’ kama alivyofanya Daudi, tutaona uthibitisho wa nguvu zake kila mahali—katika pepo na mawimbi, katika ngurumo na radi, katika mito mikubwa na milima yenye fahari. (Zaburi 111:2; Ayubu 26:12-14) Na zaidi, kama Yehova alivyomkumbusha Yobu, wanyama hushuhudia nguvu Zake. Miongoni mwa wanyama hao mna Behemothi, au kiboko. Yehova alimwambia Yobu: “Nguvu zake ni katika viuno vyake . . . Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.” (Ayubu 40:15-18) Katika nyakati za Biblia fahali wa mwitu alijulikana sana kuwa mwenye nguvu za kutisha, na Daudi alisali ili aokolewe kutokana na “kinywa cha simba, na pembe za fahali wa mwitu.”—Zaburi 22:21, NW; Ayubu 39:9-11.

      6. Fahali hufananisha nini katika Maandiko, na kwa nini? (Ona kielezi-chini.)

      6 Kwa sababu ya nguvu zake, fahali hutumiwa katika Biblia kufananisha uwezo wa Yehova.c Ono la mtume Yohana la kiti cha enzi cha Yehova laonyesha viumbe-hai wanne, na mmojawapo ana uso kama fahali. (Ufunuo 4:6, 7) Inaonekana kwamba mojawapo ya sifa kuu nne za Yehova zinazoonyeshwa na makerubi hao ni nguvu. Sifa nyinginezo ni upendo, hekima, na haki. Kwa kuwa nguvu ni sehemu muhimu sana ya utu wa Mungu, kufahamu vizuri nguvu zake na jinsi anavyozitumia kutatuvuta karibu zaidi naye na kutusaidia kuiga mfano wake kwa kutumia vizuri nguvu zetu.—Waefeso 5:1.

  • Yehova—Mungu Aliye Hodari kwa Nguvu Zake
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Machi 1
    • c Yaelekea kwamba fahali wa mwitu anayetajwa katika Biblia ni auroch (Kilatini urus). Miaka elfu mbili iliyopita, wanyama hawa waliishi Gaul (ambayo sasa ni Ufaransa), na Juliasi Kaisari aliandika hivi juu yao: “Wanyama hao, uri, karibu watoshane na tembo, lakini tabia yao, rangi yao na umbo lao ni kama fahali. Wana nguvu nyingi sana, na wana mbio sana: hawamwachi mtu wala mnyama mara wanapowaona.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki