-
Ufanisi Waweza Kutahini Imani YakoMnara wa Mlinzi—1993 | Julai 15
-
-
Ingawa Asafu alijua juu ya wema wa Yehova, miguu yake ilikuwa karibu kupotoka kutoka kwenye kijia cha uadilifu. Ilikuwa kana kwamba inateleza kwenye ardhi yenye barafu wakati wa mashindano ya mbio ndefu yenye kuchosha. Kwa nini imani yake ilikuja kuwa dhaifu hivyo? Alieleza hivi: “Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna, nilipoiona hali ya amani ya wasio haki. Maana hawana maumivu katika kufa kwao, na mwili wao una nguvu. Katika taabu ya watu hawamo, wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.”—Zaburi 73:3-5.
-
-
Ufanisi Waweza Kutahini Imani YakoMnara wa Mlinzi—1993 | Julai 15
-
-
Watu wengi waovu hawana matatizo ya afya yanayowazuia wasifurahie ugavi wao mwingi wa chakula. “Mwili wao una nguvu [vitambi vyao vimenenepa, NW],” matumbo yao makubwa yakitokeza. Zaidi ya hayo, “katika taabu ya watu hawamo,” kwani tofauti na ainabinadamu kwa ujumla, hawahitaji kung’ang’ania mahitaji ya kila siku. Asafu alimalizia kwamba waovu “hawapati mapigo pamoja na wanadamu.” Wao hasa huepuka majaribu ambayo watu wenye kumcha Mungu hupata kwa sababu hao wa pili hufuata viwango vya Yehova vyenye uadilifu katika ulimwengu mwovu wa Shetani.—1 Yohana 5:19.
-