-
Ufanisi Waweza Kutahini Imani YakoMnara wa Mlinzi—1993 | Julai 15
-
-
Aking’amua mwishoni kwamba fikira zake hazikufaa, Asafu alisema hivi: “Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; kumbe! ningaliwadanganya kizazi cha wana wako. Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; ikawa taabu machoni pangu; hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, nikautafakari mwisho wao. Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, huwaangusha mpaka palipoharibika. Namna gani wamekuwa ukiwa mara! Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho. Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka, uondokapo utaidharau sanamu yao.”—Zaburi 73:15-20.
-
-
Ufanisi Waweza Kutahini Imani YakoMnara wa Mlinzi—1993 | Julai 15
-
-
Asafu alikuja kung’amua kwamba Mungu alikuwa amewaweka waovu “penye utelezi.” Kwa sababu maisha yao yanategemea vitu vya kimwili, wana hatari ya kupatwa na anguko la ghafula. Mwisho kabisa, watakufa wanapozeeka, na utajiri waliopata kwa njia isiyofaa hautawapa maisha marefu zaidi. (Zaburi 49:6-12) Ufanisi wao utakuwa kama ndoto inayopita upesi. Huenda hata hukumu ikawafikia kabla yao kuzeeka wanapovuna walichopanda. (Wagalatia 6:7) Kwa kuwa wamempuuza kimakusudi Yule pekee awezaye kuwasaidia, wanaachwa hoi, bila tumaini. Yehova anapotenda dhidi yao, ataiona “sanamu” yao—fahari na cheo chao—kwa madharau.
-