-
Yehova Hutujulisha Jinsi ya Kuzihesabu Siku ZetuMnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 15
-
-
9. Mtunga-zaburi analinganisha kipindi cha miaka elfu ya kuwepo kwa wanadamu na nini?
9 Mtunga-zaburi alipuliziwa kuonyesha kwamba kipindi cha miaka elfu cha kuwepo kwa wanadamu ni muda mfupi sana machoni pa Muumba wa milele. Alimwambia Mungu hivi: “Wamrudisha mtu mavumbini [“wamrudisha mwanadamu awezaye kufa kuwa kitu kilichopondwa,” “NW”], usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikiisha kupita, na kama kesha la usiku.”—Zaburi 90:3, 4.
-
-
Yehova Hutujulisha Jinsi ya Kuzihesabu Siku ZetuMnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 15
-
-
11. Kwa nini tunaweza kusema kwamba muda unaoonekana kuwa mrefu sana kwetu ni mfupi sana kwa Mungu?
11 Kwa maoni ya Yehova, hata Methusela aliyekuwa na umri wa miaka 969 aliishi kwa muda unaopungua siku moja. (Mwanzo 5:27) Kwa Mungu miaka elfu ni kama siku ya jana—muda wa saa 24 tu—ikiisha kupita. Mtunga-zaburi pia anataja kwamba kwa Mungu miaka elfu ni kama muda wa saa nne ambazo mlinzi anakuwa kambini wakati wa usiku. (Waamuzi 7:19) Basi, ni wazi kwamba muda unaoonekana kuwa mrefu sana kwetu ni mfupi sana kwa Yehova, Mungu wa milele.
-