Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Linda Moyo Wako”
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 15
    • Akikumbuka ushauri wenye upendo wa baba yake, Solomoni asimulia: “Naye akanifundisha, akaniambia, moyo wako uyahifadhi maneno yangu; shika amri zangu ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu [“uelewevu,” “NW”]; usiusahau; wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Usimwache [hekima], naye atakuhifadhi; umpende, naye atakulinda. Bora hekima, basi jipatie hekima; naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu [“uelewevu,” “NW”].”—Mithali 4:4-7.

  • “Linda Moyo Wako”
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 15
    • Kupata uelewevu ni muhimu pia. Bila uelewevu, je, tunaweza kuona jinsi mambo yanavyohusiana na kupata kuelewa kikamili jambo tunalochunguza? Kama hatuna uelewevu, tunawezaje kujua sababu zinazofanya mambo yafanyike kwa njia fulani na kupata ufahamu wenye kina na utambuzi? Naam, tunahitaji uelewevu ili tuweze kusababu kutokana na mambo tujuayo kisha kuamua mambo ifaavyo.—Danieli 9:22, 23.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki