-
Pata Hekima na Ukubali NidhamuMnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
Kusudi la kitabu cha Mithali limefafanuliwa katika maneno yake ya ufunguzi: “Mithali za Sulemani [“Solomoni,” “NW”]; mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu [“nidhamu,” “NW”]; kutambua maneno ya ufahamu [“uelewevu,” “NW”]; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari.”—Mithali 1:1-4, italiki ni zetu.
-
-
Pata Hekima na Ukubali NidhamuMnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
Hekima yahusisha mambo mengi, kutia ndani uelewevu, ufahamu wenye kina, werevu, na uwezo wa kufikiri. Uelewevu ni uwezo wa kuchunguza jambo na kupambanua muundo wake kwa kujua uhusiano kati ya sehemu zake mbalimbali na kati ya muundo wote mzima, hivyo kulielewa. Ufahamu wenye kina wahitaji mtu ajue sababu na kuelewa ni kwa nini mwenendo fulani ni mbaya au ni mzuri. Kwa mfano, mtu mwenye uelewevu aweza kufahamu mtu anapokengeuka, na huenda mara moja akamwonya kuhusu hatari ya kufanya hivyo. Lakini anahitaji ufahamu wenye kina kutambua ni kwa nini mtu huyo anakengeuka na kutokeza njia ifaayo zaidi ya kumwokoa.
-