Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 8/1 uku. 32
  • “Mke wa Ujana Wako”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mke wa Ujana Wako”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 8/1 uku. 32

“Mke wa Ujana Wako”

“UZINZI karibu waonekana kuwa tukio la kila siku.” Ndivyo wasemavyo wastadi wengi, kulingana na Los Angeles Times. Je! maneno hayo yanakushangaza? Hata hivyo, daktari wa ugonjwa wa akili Frank Pittman hukadiri kwamba karibu asilimia 50 ya waume na kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40 ya wake hawajawa waaminifu. Ikiwa hilo ni kweli, karibu nusu ya watu wote waliofunga ndoa hufanya uzinzi!

Je! hilo lamaanisha kwamba ukosefu wa adili unafaa? Hasha! Mweneo wa uzini hauufanyi ufae—jinsi ambavyo ongezeko la uhalifu mtaani halifanyi kumnyang’anya mtu kitu kufae. Ukosefu wa adili huumiza. Kwa mfano, ainabinadamu leo imepatwa na mweneo wa magonjwa ya hatari yenye kuambukizwa kingono yote ambayo yangeweza kudhibitiwa kwa urahisi ikiwa watu wangekuwa na maisha ya kiadili. Ule ugonjwa UKIMWI uuao usingalikuwa na uwezo wa kuenea sana jinsi ulivyo navyo ikiwa watu wasingalikuwa walegevu sana katika maisha yao ya kingono.

Isitoshe, hata wale walio wa kimambo-leo na “wenye kutiwa nuru” zaidi huhisi uchungu mwingi wakati wenzi wao wasipokuwa waaminifu. Tendo moja la uzinzi laweza kusababisha majeraha yanayochukua muda mrefu sana kuponywa.

Hata hivyo, jambo la maana sana ni kwamba kutochukua nadhiri za ndoa kwa uzito ni ukosefu mbukwa sana wa kuonyesha staha kwa Mungu. kwa kuwa yeye ndiye Mwanzilishi wa ndoa. Biblia husema hivi: “Ndoa na iheshimiwe na watu wote.” Tunaonywa hivi pia: “Waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”—Waebrania 13:4.

Kwa hiyo, watu wenye hekima hutii maneno haya yaliyopuliziwa roho: “Umfurahie mke wa ujana wako.” (Mithali 5:18) Wao hutafuta uradhi na furaha kwa wenzi wao wa ndoa. Kwa kufanya hivyo wao hulinda afya yao ya kimwili na ya kihisiamoyo, na la maana zaidi, wao humletea heshima yule Mwanzilishi mkuu wa ndoa, Yehova Mungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki