-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
Kwa maneno yaliyo kama ya baba mwenye upendo, Mfalme Solomoni wa Israeli la kale ambaye alikuwa mwenye hekima, asema: “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; naam, ukiita busara [“uelewevu,” “NW”], na kupaza sauti yako upate ufahamu; ukiutafuta kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, na kupata kumjua Mungu.”—Mithali 2:1-5.
-
-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
Hekima ni uwezo wa kutumia ifaavyo ujuzi tuliyopewa na Mungu. Nayo Biblia hutuwezesha kupata hekima kwa njia nzuri kama nini! Naam, ina maneno ya hekima, kama yale yaliyorekodiwa katika vitabu vya Mithali na Mhubiri, nasi twahitaji kuyakazia uangalifu. Katika Biblia sisi hupata pia mifano mingi ambayo huonyesha manufaa za kutumia kanuni za kimungu na hatari ya kuzipuuza. (Waroma 15:4; 1 Wakorintho 10:11) Kwa mfano, fikiria masimulizi juu ya Gehazi mwenye pupa, aliyekuwa mhudumu wa nabii Elisha. (2 Wafalme 5:20-27) Je, hayatufundishi hekima ya kuepuka pupa? Na namna gani matokeo yenye msiba ya ziara ambazo hazikuonekana kuwa hatari, wakati Dina binti ya Yakobo alipokuwa akiwazuru “binti za nchi” ya Kanaani? (Mwanzo 34:1-31) Je, hatutambui kwa urahisi upumbavu wa kuwa na mashirika mabaya?—Mithali 13:20; 1 Wakorintho 15:33.
Kuzingatia hekima kwahusisha kujifunza ufahamu na uelewevu. Kwa mujibu wa Webster’s Revised Unabridged Dictionary, ufahamu ni “nguvu au uwezo unaowezesha akili kupambanua mambo.” Ufahamu wa kimungu ni uwezo wa kupambanua mema na mabaya, kisha kuchagua mwenendo ufaao. ‘Tusipoielekeza mioyo’ yetu ipate ufahamu au tusipokuwa na hamu ya kujipatia ufahamu huo, tunawezaje kukaa katika ‘barabara iongozayo kuingia katika uhai’? (Mathayo 7:14; linganisha Kumbukumbu la Torati 30:19, 20.) Kujifunza na kutumia Neno la Mungu hutupa ufahamu.
-