Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Bwana Huwapa Watu Hekima”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
    • Kwa maneno yaliyo kama ya baba mwenye upendo, Mfalme Solomoni wa Israeli la kale ambaye alikuwa mwenye hekima, asema: “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; naam, ukiita busara [“uelewevu,” “NW”], na kupaza sauti yako upate ufahamu; ukiutafuta kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, na kupata kumjua Mungu.”—Mithali 2:1-5.

  • “Bwana Huwapa Watu Hekima”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
    • Fikiria hazina kubwa tutakazopata ikiwa kwa moyo mnyofu tunachimba sana katika Biblia. Kwani, tutapata “kumjua Mungu”—ujuzi kumhusu Muumba wetu ambao ni imara na wenye kutuletea uhai! (Yohana 17:3) ‘Kumcha BWANA’ pia ni hazina tuwezayo kujipatia. Kicho hicho chenye staha kina thamani iliyoje! Hofu ifaayo ya kutomkasirisha yapaswa iongoze maisha yetu yote, ikiongezea maana ya kiroho yale yote tufanyayo.—Mhubiri 12:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki