Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nitashughulikaje na Watu Wenye Hasira?
    Amkeni!—2001 | Novemba 22
    • “Alikuwa na hasira kali. Nafikiri alitaka kunipiga kwa sababu aliona nilikuwa mdogo. Nilipokuwa nikisonga nyuma, nilisema: ‘Hebu ngoja! Ngoja kidogo! Ngoja kidogo! Mbona unataka kunipiga? Sijakufanya lolote. Hata sijui umekasirishwa na nini. Je, twaweza kusuluhisha jambo hilo?’”—David, mwenye umri wa miaka 16.

  • Nitashughulikaje na Watu Wenye Hasira?
    Amkeni!—2001 | Novemba 22
    • Biblia hutoa shauri hili la hekima: “Jawabu la upole hugeuza hasira; bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.” (Mithali 15:1) Naam, ukisema “neno liumizalo” wakati mtu anapokukasirikia, jambo hilo litafanya hali iwe mbaya zaidi. Hata hivyo, mara nyingi jawabu la upole laweza kutuliza mambo na kumaliza uhasama.

      Kumbuka David aliyetajwa mwanzoni. Alimwomba yule mchokozi amweleze ni nini kilichomkasirisha. Mtu fulani alikuwa ameiba chakula chake cha mchana, na alimfokea tu mtu aliyekutana naye kwanza. David alimwambia hivi: “Hutapata chakula chako cha mchana kwa kunipiga.” Kisha David akapendekeza waende kwenye mkahawa. David alisema hivi: “Kwa kuwa nilimjua muuzaji kwenye mkahawa huo, nilimsaidia apate chakula kingine. Alinishukuru, na baada ya hapo akawa mwenye urafiki.” Je, waona jinsi maneno ya upole yalivyo na nguvu? Kama mithali moja inavyosema, “ulimi laini [mpole, NW] huvunja mfupa.”—Mithali 25:15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki