-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
Twashukuru kama nini kwamba hekima ya kweli na sifa zinazohusiana nayo pia hutulinda dhidi ya njia mbaya ya wanaume na wanawake wasio waadilifu! Solomoni aongezea kwamba sifa hizo ‘zitakuokoa na malaya [“mwanamke mgeni,” “NW”], naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake; amwachaye rafiki wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Maana nyumba yake inaelekea mauti, na mapito yake yanakwenda kwenye wafu. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, wala hawazifikilii njia za uzima.’—Mithali 2:16-19.
Huyo malaya, “mwanamke mgeni,” anasemwa kuwa mwanamke aachaye “rafiki wa ujana wake”—yaelekea mume wa ujana wake.a (Linganisha Malaki 2:14.) Amesahau ile sehemu ya agano la Sheria inayokataza uzinzi. (Kutoka 20:14) Njia zake zinaelekea kwenye kifo. Wanaoshirikiana naye huenda wasiweze kamwe ‘kuzifikilia njia za uzima,’ kwa kuwa huenda siku moja wakafikia hatua ambayo hali yao haiwezi kurekebishwa, yaani kifo, ambacho hakiwezi kubadilishwa. Mtu wa ufahamu na busara anajua mitego ya ukosefu wa adili naye huepuka kwa hekima kunaswa nayo.
-
-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
[Maelezo ya Chini]
a Neno “mgeni” lilitumiwa kuwahusu wale waliokiuka Sheria, hivyo wakajitenga na Yehova. Hivyo, malaya—na si lazima mtu wa kutoka nchi ya kigeni—anaitwa “mwanamke mgeni.”
-