Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dumisha Maoni Yaliyosawazika Kuhusu Kutumia Kileo
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 1
    • 2. Tutazungumzia maswali gani kuhusu kutumia kileo?

      2 Zawadi inayofurahisha huwa nzuri inapotumiwa tu kwa njia inayofaa. Kwa mfano, asali “ni njema” lakini “si vizuri kula asali nyingi mno.” (Methali 24:13; 25:27) Ingawa huenda ikafaa kunywa “divai kidogo,” kutumia kileo vibaya ni tatizo kubwa. (1 Timotheo 5:23) Biblia huonya hivi: “Divai ni mdhihaki, kileo husababisha msukosuko, na kila mtu anayepotezwa nacho hana hekima.” (Methali 20:1) Hata hivyo, mtu anawezaje kupotezwa na kileo?a Ni kiwango gani cha divai kinachopita kiasi? Ni maoni gani yaliyosawazika kuhusiana na jambo hilo?

      ‘Mtu Anawezaje Kupotezwa’ na Kileo?

      3, 4. (a) Ni nini kinachoonyesha kwamba Biblia hushutumu kunywa kileo mpaka mtu alewe? (b) Ni nini baadhi ya dalili za ulevi?

      3 Katika Israeli la kale, mwana aliyekuwa mlafi na mlevi asiyetubu alipaswa kuuawa kwa kupigwa mawe. (Kumbukumbu la Torati 21:18-21) Mtume Paulo aliwaonya Wakristo hivi: “Mwache kuchangamana katika ushirika pamoja na mtu yeyote anayeitwa ndugu ambaye ni mwasherati au mtu mwenye pupa au mwabudu-sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi, hata msile chakula pamoja na mtu wa namna hiyo.” Ni wazi kwamba Maandiko yanashutumu kunywa kileo mpaka mtu alewe.—1 Wakorintho 5:11; 6:9, 10.

      4 Ikieleza dalili za ulevi, Biblia husema: “Usiitazame divai inapotoa rangi nyekundu, inapochemka katika kikombe, inaposhuka taratibu. Mwisho wake inauma kama nyoka, nayo hutoa sumu kama nyoka. Macho yako mwenyewe yataona mambo mageni, nao moyo wako mwenyewe utasema mambo yaliyopotoka.” (Methali 23:31-33) Kunywa kupita kiasi huuma kama nyoka mwenye sumu na kusababisha ugonjwa, kuvurugika kiakili na hata kupoteza fahamu. Mlevi anaweza kuona “mambo mageni” katika maana ya kwamba anaweza kusikia sauti zisizokuwepo au kuota ndoto za mchana. Huenda pia akakosa kujizuia kusema na kufanya mambo yaliyopotoka ambayo kwa kawaida hangefanya.

      5. Kunywa kileo kupita kiasi ni hatari jinsi gani?

      5 Namna gani ikiwa mtu anakunywa kileo lakini anakuwa mwangalifu asinywe kupita kiasi ili wengine wasione kwamba amelewa? Watu fulani hawaonyeshi sana dalili za kulewa hata baada ya kunywa sana. Hata hivyo, kufikiri kwamba zoea hilo halina madhara ni kujidanganya. (Yeremia 17:9) Hatua kwa hatua, huenda mtu akawa mzoefu wa kileo na kuwa ‘mtumwa wa divai nyingi sana.’ (Tito 2:3) Mwandishi Caroline Knapp anasema hivi kuhusu jinsi mtu huwa mzoefu wa kileo: “Mtu huwa mzoefu polepole, hatua kwa hatua, na kisiri-siri.” Kwa kweli, kutumia kileo kupita kiasi ni mtego usioonekana.

      6. Kwa nini mtu anapaswa kujiepusha kula na kunywa kileo kupita kiasi?

      6 Pia fikiria onyo hili la Yesu: “Jiangalieni ninyi wenyewe kwamba mioyo yenu isilemewe kamwe na kula kupita kiasi na kunywa sana na mahangaiko ya maisha, na kwa ghafula siku hiyo iwe juu yenu mara moja kama mtego. Kwa maana itakuja juu ya wale wote wanaokaa juu ya uso wa dunia yote.” (Luka 21:34, 35) Si lazima mtu anywe mpaka alewe kabla ya kuanza kusinzia na kuwa mvivu—kimwili na kiroho pia. Itakuwaje siku ya Yehova ikimpata katika hali hiyo?

  • Dumisha Maoni Yaliyosawazika Kuhusu Kutumia Kileo
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 1
    • 10. Kileo kinaweza kuathirije akili yetu, na kwa nini jambo hilo ni hatari?

      10 Kutumia kileo kupita kiasi hudhuru watu kimwili na kiroho pia. Biblia inasema: “Divai na divai tamu ndivyo vinavyoondoa kusudi jema.” (Hosea 4:11) Kileo huathiri akili. “Mtu anapokunywa,” chasema kichapo kimoja cha Taasisi ya Kitaifa ya Dawa za Kulevya ya Marekani, “kileo hufyonzwa kupitia mfumo wa kumeng’enya chakula hadi kwenye damu na kufika haraka kwenye ubongo. Kinaanza kufanya sehemu za ubongo ambazo hudhibiti fikira na hisia zifanye kazi polepole. Mtu hushindwa kujidhibiti.” Katika hali hiyo, ni rahisi ‘tupotee,’ tujiendeshe kwa njia isiyofaa na watu wa jinsia tofauti, na kutumbukia katika vishawishi vingi.—Methali 20:1.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki