Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Paradiso Yarudishwa!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Nchi Yenye Ukiwa Yafurahi

      3. Kulingana na unabii wa Isaya, nchi itageuzwa iweje?

      3 Unabii wa Isaya uliopuliziwa kuhusu Paradiso iliyorudishwa waanza kwa maneno haya: “Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA [“Yehova,” “NW”], ukuu wa Mungu wetu.”—Isaya 35:1, 2.

      4. Nchi ya Wayahudi yageuka kuwa kama nyika wakati gani na jinsi gani?

      4 Isaya aandika maneno hayo karibu mwaka wa 732 K.W.K. Miaka ipatayo 125 baadaye, Wababiloni waharibu Yerusalemu na watu wa Yuda wapelekwa uhamishoni. Nchi yao yaachwa ukiwa, bila watu. (2 Wafalme 25:8-11, 21-26) Basi onyo la Yehova kwamba watu wa Israeli wangeenda uhamishoni iwapo wangekosa kuwa waaminifu latimia. (Kumbukumbu la Torati 28:15, 36, 37; 1 Wafalme 9:6-8) Taifa la Waebrania linapokuwa mateka katika nchi ya kigeni, mashamba yao ya matunda yenye kunyunyizwa maji vizuri yaachwa pasipo utunzaji kwa miaka 70 nayo yawa kama nyika.—Isaya 64:10; Yeremia 4:23-27; 9:10-12.

      5. (a) Hali za kiparadiso zarudishwaje nchini? (b) Watu wauonaje “utukufu wa Yehova”?

      5 Hata hivyo, unabii wa Isaya watabiri kuwa nchi haitakaa ukiwa milele. Itarudishwa kuwa paradiso kwelikweli. Itapewa “uzuri wa Lebanoni” na “utukufu wa Karmeli na Sharoni.”a Jinsi gani? Warudipo kutoka uhamishoni, Wayahudi waweza tena kulima na kunyunyiza maji mashamba yao, na nchi yao yaanza kuzaa kwa wingi tena kama hapo awali. Ni Yehova peke yake anayestahili kusifiwa kwa hayo. Wayahudi wapata kufurahia hali hizo zinazofanana na paradiso kwa sababu ya mapenzi, utegemezo, na baraka zake. Watu waweza kuona “utukufu wa Yehova, ukuu wa Mungu [wao]” wanapoona jinsi ambavyo Yehova ameigeuza nchi yao kwa njia ya ajabu.

      6. Watu waona utimizo gani muhimu wa maneno ya Isaya?

      6 Ijapokuwa hivyo, kuna utimizo muhimu zaidi wa maneno ya Isaya katika nchi ya Israeli iliyorudishwa. Kwa miaka mingi, Israeli imekuwa katika hali ya ukame, iliyo kama jangwa kiroho. Wahamishwa walipokuwa huko Babiloni, ibada safi ilizuiwa sana. Hapakuwa na hekalu, wala madhabahu, wala ukuhani uliopangwa. Dhabihu za kila siku zilikuwa zimekoma kwa muda. Isaya sasa atoa unabii wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa watu kama vile Zerubabeli, Ezra, na Nehemia, wawakilishi kutoka kwa makabila yote 12 ya Israeli warudi Yerusalemu, wajenga tena hekalu, na kumwabudu Yehova kwa uhuru. (Ezra 2:1, 2) Hiyo ni paradiso ya kiroho kwelikweli!

  • Paradiso Yarudishwa!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Maandiko yafafanua Lebanoni ya kale kuwa nchi yenye kuzaa sana iliyo na misitu mizuri na mierezi mikubwa, kama ilivyokuwa Bustani ya Edeni. (Zaburi 29:5; 72:16; Ezekieli 28:11-13) Sharoni ilikuwa maarufu kwa sababu ya vijito na misitu yake ya mialoni; Karmeli ilikuwa maarufu kwa sababu ya mashamba yake ya mizabibu, matunda, na miteremko yenye kujaa maua.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki