Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 9/15 uku. 32
  • Kama Panzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kama Panzi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 9/15 uku. 32

Kama Panzi

JE! UMEPATA kutembea polepole ukivuka shamba la majani katika kiangazi na kuona panzi wengi sana wakiruka kutoka njiani mwako? Walionekana kuwa kila mahali, ingawa huenda ikawa hukuwakazia fikira sana. Kwa vyovyote, wanaonekana kuwa wasiodhuru na duni.

Lakini, uduni hasa wa panzi ndio huwafanya kuwa mfano ufaao wa ainabinadamu. Ingawa watu fulani mashuhuri huenda wakajiona wenyewe kuwa wa maana sana, Muumba wetu huona vingine. Nabii wake Isaya alisema hivi: “Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi.”—Isaya 40:22.

Ukuu, uwezo, na hekima ya Yehova Mungu, humwinua juu zaidi ya makao ya wanadamu walio duni, kama vile mwanadamu alivyo mkuu zaidi kuliko panzi katika akili na nguvu. Hata hivyo, sifa kuu zaidi ya Mungu ni upendo. Na upendo wake usio na kifani humsukuma kutufikiria, kutusaidia, na kutuokoa—tukimpenda na kumtii. Yehova hushughulika nasi kwa upendo, hata ingawa sisi ni kama panzi walio duni. Mtunga-zaburi alisema hivi: “Ni nani aliye mfano wa BWANA [Yehova, NW], Mungu wetu aketiye juu; anyenyekeaye kutazama, mbinguni na duniani? Humwinua mnyonge kutoka mavumbini.”—Zaburi 113:5-7.

Kama zaburi hiyo ielezavyo, Yehova kwa upendo hutoa msaada kwa yule aliye mnyonge. Naam, Yeye huwasaidia wale ‘wanaomtafuta Mungu na kwa kweli wampate.’ (Matendo 17:27, NW) Wale wanaompata Mungu—na kumtumikia—hata huwa wenye thamani kubwa machoni pake. (Linganisha Isaya 43:4, 10.) Hivyo panzi mdogo hutumika kutukumbusha juu ya uduni wetu wenyewe na juu ya upendo wa Muumba wetu mweza yote, anayewapa wanadamu watiifu urafiki wake na fadhili yake isiyostahiliwa. Je! wewe unaonyesha uthamini kwa ajili ya upendo wa Mungu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki