-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
d Tai huelea kwa kutumia nguvu kidogo sana. Yeye hufanya hivyo akitumia kwa ustadi mawimbi yanayoinuka ya hewa joto.
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 404, 405]
Yehova, Mchungaji Mwenye Upendo
Ili kuonyesha jinsi Yehova anavyowahangaikia watu wake, Isaya amfananisha Yehova na mchungaji anayebeba wana-kondoo wake kifuani mwake. (Isaya 40:10, 11) Yaonekana mfano huo wa Isaya ulitegemea mazoea halisi ya wachungaji wa kale. Fikiria kielelezo cha karibuni zaidi. Mtazamaji aliyewatazama wachungaji kwenye miteremko ya Mlima Hermoni katika Mashariki ya Kati asema jinsi wanavyotunza kondoo zao kwa wororo. “Kila mchungaji aliangalia kwa makini kundi lake ili kuona jinsi linavyoendelea. Akipata mwana-kondoo aliyezaliwa hivi karibuni, angemweka katika mikunjo ya . . . kanzu yake kubwa, kwa kuwa alikuwa dhaifu sana asiuweze mwendo wa mama yake. Kifua chake kilipojaa, aliwaweka wana-kondoo mabegani mwake, akiwashika kwa miguu, au kwenye mfuko au kikapu mgongoni mwa punda, hadi kondoo wachanga wauweze mwendo wa mama zao.” Je, haifariji kujua kuwa twamtumikia Mungu anayewahangaikia watu wake kwa wororo?
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 412]
Dunia Ina Umbo Gani?
Nyakati za kale, wanadamu kwa jumla waliamini kwamba dunia ni tambarare. Hata hivyo, mapema katika karne ya sita K.W.K., mwanafalsafa Mgiriki aitwaye Pythagoras alikisia-kisia kwamba dunia ni mviringo. Licha ya hayo, karne mbili kabla ya Pythagoras kutunga nadharia yake, nabii Isaya alitaarifu hivi kwa uwazi na uhakika wa ajabu: “Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia.” (Isaya 40:22, italiki ni zetu.) Neno la Kiebrania chugh ambalo hapa limetafsiriwa “duara” laweza kufasiriwa “mviringo.” Chombo cha mviringo ndicho pekee kionekanacho kama duara pande zote.e Basi muda mrefu mapema, nabii Isaya aliandika taarifa ambayo ni sahihi kisayansi na isiyoathiriwa na ngano za kale.
[Maelezo ya Chini]
e Kihalisi, dunia ina umbo la mviringo wenye mbenuko. Ni tambarare kidogo pembeni.
[Picha katika ukurasa wa 403]
Yohana Mbatizaji alikuwa sauti ya mtu ‘apaazaye kilio nyikani’