Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 2 Mfano wa Isaya waanza hivi: “Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, kilimani penye kuzaa sana; akafanya handaki kulizunguka pande zote, akatoa mawe yake, akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, akajenga mnara katikati yake, akachimba shinikizo ndani yake; akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, nao ukazaa zabibu-mwitu.”—Isaya 5:1, 2; linganisha Marko 12:1.

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 4 Kazi ngumu yahitajika ili shamba la mizabibu lizae. Isaya aeleza kuwa mmilikaji ‘afanya handaki [“alililima vizuri,” BHN] shamba na kutoa mawe yake’—kazi ngumu, yenye kuchosha sana! Yaelekea atumia mawe yaliyo makubwa ‘kujenga mnara.’ Nyakati za kale, minara hiyo ilikuwa vituo vya walinzi walioilinda mimea dhidi ya wezi na wanyama.a Pia, ajenga ukuta wa mawe ili kuyazunguka matuta ya shamba hilo la mizabibu. (Isaya 5:5) Mara nyingi hilo lilifanywa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo wa juu ulio muhimu.

      5. Mmilikaji atarajia nini kwa kufaa kutoka kwa shamba lake la mizabibu, lakini yeye apata nini?

      5 Baada ya kufanya kazi kwa bidii ili kulilinda shamba lake la mizabibu, mmilikaji ana haki ya kulitazamia lizae matunda. Kwa kutazamia hilo, yeye achimba shinikizo la divai. Lakini je, mavuno yanayotarajiwa yatokea? La, shamba hilo la mizabibu lazaa zabibu-mwitu.

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Wasomi fulani huamini kuwa majengo ya bei rahisi na ya muda mfupi, kama vile mahema, au vibanda, yalitumiwa mara nyingi kuliko minara ya mawe. (Isaya 1:8) Kuwepo kwa mnara kungeonyesha kuwa mwenye-shamba amelifanyia “shamba lake la mizabibu” kazi kubwa zaidi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki