-
“Ninyi Ni Mashahidi Wangu”!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
11. Ni agizo gani ambalo Yehova anampa mtumishi wake, na Yehova anafunua nini juu ya Uungu wake?
11 Miungu ya uwongo haiwezi kutokeza mashahidi maana haiwezi kitu. Basi aibu ndiyo hiyo, kizimba cha ushahidi kinabaki tupu. Lakini sasa ni wakati wa Yehova kuthibitisha Uungu wake. Akiwatazama watu wake, anasema hivi: “Ninyi ni mashahidi wangu, . . . na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni BWANA [“Yehova,” “NW”], zaidi yangu mimi hapana mwokozi. Nimetangaza habari, nimeokoa, nimeonyesha, na hapakuwa mungu wa kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni mashahidi wangu, . . . nami ni Mungu. Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye [kuuzuia mkono wangu]?”—Isaya 43:10-13.
-
-
“Ninyi Ni Mashahidi Wangu”!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
14. Yehova anawakumbusha nini Waisraeli, na kwa nini kikumbusha hicho ni cha wakati unaofaa?
14 Yehova anawajali wale wanaoitwa kwa jina lake huku wakililetea heshima, na anawaona “kama mboni ya jicho” lake. Anawakumbusha Waisraeli hivyo kwa kuwaeleza jinsi alivyowakomboa kutoka Misri, akawaongoza salama kuvuka jangwa. (Kumbukumbu la Torati 32:10, 12) Wakati huo hakukuwa na mungu wa kigeni kati yao, maana walijionea miungu ya Misri ikiaibishwa kabisa. Ndiyo, miungu yote ya Misri haikuweza kulinda Misri wala kuzuia Israeli wasiondoke. (Kutoka 12:12) Vivyo hivyo, Babiloni hodari, ambayo ina mji wenye angalau mahekalu 50 ya miungu ya uwongo, haitaweza kuzuia mkono wa Mweza Yote anapowaweka huru watu wake. Ni wazi “hapana mwokozi” zaidi ya Yehova.
-