-
Kumtambua Mjumbe wa Aina InayofaaMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
-
-
“Nami ndiye . . . Yule afanyaye neno la mtumishi wake litimie, na Yule ambaye hutekeleza kikamili shauri la wajumbe wake mwenyewe.”—ISAYA 44:25, 26, NW.
1. Yehova hutambuaje wajumbe wa aina inayofaa, naye huwafichuaje wasio wa kweli?
YEHOVA MUNGU ndiye Mtambuaji Mtukufu wa wajumbe wake wa kweli. Huwatambua kwa kufanya ujumbe mbalimbali anaotoa kupitia wao utimie. Yehova pia ndiye Mfichuaji Mkuu wa wajumbe wasio wa kweli. Yeye huwafichuaje? Hubatilisha ishara na matabiri yao. Kwa njia hiyo yeye huonyesha kwamba wao ni watabiri waliojiweka rasmi wenyewe, ambao ujumbe wao mbalimbali kwa kweli hutokana na kufikiri kwao wenyewe kusiko kwa kweli—ndiyo, kufikiri kwao kwa kipumbavu, kwa kimwili!
-
-
Kumtambua Mjumbe wa Aina InayofaaMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
-
-
6 Kana kwamba hilo halikutosha, Waisraeli waliokuwa mateka walipatwa pia na maoni ya watabiri wenye kujivuna, waaguzi, na wanajimu wa Babiloni. Hata hivyo, Yehova aliwathibitisha wajumbe wote hao wasio wa kweli kuwa wapumbavu walioshindwa, wenye kutoa unabii kinyume cha kile ambacho kingetukia. Kwa wakati ufaao yeye alionyesha kwamba Ezekieli alikuwa mjumbe wake wa kweli, kama alivyokuwa Isaya. Yehova alitimiza maneno yote aliyosema kupitia wao, kama tu alivyokuwa ameahidi: “Nazibatilisha ishara za waongeao upuzi, nami ndiye Yule ambaye hufanya waaguzi wenyewe watende kwa kichaa; Yule ageuzaye watu wenye hekima nyuma, na Yule ambaye hugeuza hata ujuzi wao kuwa upumbavu; Yule afanyaye neno la mtumishi wake litimie, na Yule ambaye hutekeleza kikamili shauri la wajumbe wake mwenyewe.”—Isaya 44:25, 26, NW.
-