-
Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
25, 26. Isaya afunua hali gani mbovu ya kufikiri kwa Waisraeli katika ole wa tatu na wa nne?
25 Sasa sikiliza ole wa tatu na wa nne wa Isaya: “Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari! Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona. Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!”—Isaya 5:18-20.
26 Hiyo yawafafanua kinaganaga kama nini wale wanaozoea dhambi! Wameshikamana na dhambi kama vile wanyama wavutao mizigo wanavyofungwa kwenye magari. Watenda-dhambi hao hawaogopi siku yoyote ya hukumu inayokuja. Wao wasema kwa dhihaka: “[Mungu] na . . . aihimize kazi yake”! Badala ya kuitii Sheria ya Mungu, wao hupotoa mambo, wakitangaza kuwa “uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu.”—Linganisha Yeremia 6:15; 2 Petro 3:3-7.
-
-
Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
[Picha katika ukurasa wa 83]
Mtenda-dhambi ameshikamana na dhambi kama vile mnyama avutaye mizigo anavyofungwa kwenye gari
-