Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 19, 20. (a) Yehova anafikisha kesi yake kwenye upeo kwa njia gani? (b) Yehova anawatolea watu wake unabii wa mambo gani yenye kuchangamsha, na ni nani atakuwa mwakilishi wake wa kuyatimiza?

      19 Yehova sasa analeta hoja yake ya kisheria kwenye upeo mpevu. Yeye mwenyewe anakaribia kuujibu mtihani mkali kupita wote wa Uungu wake, yaani, kama kweli anaweza kutabiri wakati ujao kwa usahihi. Msomi mmoja wa Biblia aliiita mistari mitano inayofuata ya Isaya sura ya 44, “shairi lisilo na kifani la Mungu wa Israeli,” yule Muumba mmoja, tena mmoja tu, aliye Mfunuaji pekee wa wakati ujao na tumaini la ukombozi wa Israeli. Maelezo ya kifungu hicho yanafikia upeo wenye kuvutia sana hatua kwa hatua kwa kutangaza jina la mwanamume atakayekomboa taifa hilo kutoka Babiloni.

      20 “BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka; niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako; nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.”—Isaya 44:24-28.

  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 22. Eleza Mto Eufrati unakauka jinsi gani.

      22 Kwa kawaida waaguzi wasiopuliziwa hawathubutu kutabiri mambo hususa, kwa kuhofu kwamba watathibitishwa kuwa waongo baada ya muda. Lakini Yehova ni tofauti kwa sababu anafunua kupitia Isaya jina hususa la mwanamume ambaye Yeye atamtumia kuwaweka huru watu wake watoke utekwani, waweze kwenda nyumbani wakajenge upya Yerusalemu na hekalu. Jina lake ni Koreshi, na anajulikana kuwa Koreshi Mkuu wa Uajemi. Yehova anatoa hata maelezo madogo-madogo kuhusu maarifa ambayo Koreshi atatumia kuupenya mfumo mkubwa sana wa Babiloni ulio na kinga nyingi. Babiloni italindwa na kuta ndefu na mapito ya maji yanayotiririka ndani ya jiji na vizingo vyake. Koreshi atageuza sehemu kubwa ya mfumo huo—ule Mto Eufrati—itimize lengo lake. Kulingana na wanahistoria wa kale Herodotus na Xenophon, katika upande fulani wa juu wa Babiloni, Koreshi aliyaelekeza kando maji mengi ya Mto Eufrati maji yakapungua kiasi cha askari zake kupita kwa miguu. Eufrati unakauka kwa maana ya kwamba hauwezi kulinda Babiloni.

      23. Kuna maandishi gani ya kuonyesha utimizo wa ule unabii wa kwamba Koreshi angekomboa Israeli?

      23 Namna gani ile ahadi ya kwamba Koreshi atawafungua watu wa Mungu na kwamba atahakikisha Yerusalemu na hekalu vitajengwa upya? Koreshi mwenyewe, katika tangazo rasmi lililohifadhiwa katika Biblia, anatangaza hivi: “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.” (Ezra 1:2, 3) Ahaa! Neno la Yehova kupitia Isaya limetimizwa kabisa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki