Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 3. Isaya 45:1-3a inasimulia ushindi wa Koreshi kwa maneno gani dhahiri?

      3 “Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri.”—Isaya 45:1-3a.

      4. (a) Kwa nini Yehova anamwita Koreshi “masihi” wake? (b) Yehova atamhakikishiaje Koreshi ushindi?

      4 Yehova anamtumia Isaya kumtaja Koreshi kana kwamba yuko hai, ingawa Koreshi bado hajazaliwa siku za Isaya. (Waroma 4:17) Kwa kuwa Yehova anamweka rasmi Koreshi mapema ili atimize kazi fulani hususa, Koreshi anaweza kusemwa kuwa ni “masihi” wa Mungu. Koreshi ataongozwa na Mungu kutiisha mataifa, awadhoofishe wafalme na kuwamaliza nguvu za ukinzani. Kisha, Koreshi ashambuliapo Babiloni, Yehova atahakikisha kwamba milango ya jiji imeachwa wazi, aifanye iwe ovyo kama malango ambayo yamekwisha kuvunjwa-vunjwa. Ataenda mbele ya Koreshi, akitandaza vipingamizi vyote. Mwishowe, vikosi vya Koreshi vitalishinda jiji na kutwaa “mali zilizofichwa” humo, utajiri wake uliowekwa katika ghala za gizani. Isaya anatabiri hivyo. Je, maneno yake yanatimia?

      5, 6. Unabii wa anguko la Babiloni unatimia wakati gani na jinsi gani?

      5 Mwaka wa 539 K.W.K.—kama miaka 200 baada ya Isaya kuandika unabii huu—kwa kweli Koreshi anawasili kwenye kuta za Babiloni kushambulia jiji hilo. (Yeremia 51:11, 12) Hata hivyo, Wababiloni hawajali. Wanaona kwamba jiji lao halishindiki. Kuta zake ndefu zimeinuka sana juu ya mahandaki ya kina kirefu yaliyojaa maji ya Mto Eufrati, ambao ni sehemu ya mfumo wa kinga za jiji. Miaka zaidi ya mia moja ndiyo hiyo, na hakuna adui amefaulu kuipiga Babiloni dafrao! Kwa kweli, Belshaza, aliye mtawala mkazi wa Babiloni, anajiona salama salimini, hata anakula karamu na washiriki wa baraza lake. (Danieli 5:1) Usiku huo—huo usiku wa Oktoba 5/6—Koreshi akamilisha mbinu murua ya ushambulizi wa kijeshi.

      6 Kwenye maji ya upande wa juu kutoka Babiloni, wahandisi wa Koreshi wamepasua njia kuupita ukingo wa Mto Eufrati, wakabadili mkondo wa maji yake mengi, na sasa hayatiririki tena kusini kuelekea jijini. Muda si muda, maji ya mto yaliyo ndani ya Babiloni na vizingo vyake yamepunguka sana hivi kwamba vikosi vya Koreshi vyaweza kupita chubwichubwi katika sakafu ya mto, kuelekea kitovu cha jiji hilo. (Isaya 44:27; Yeremia 50:38) Jamani, malango kando ya mto yako wazi, sawasawa na utabiri wa Isaya. Majeshi ya Koreshi yamiminika Babiloni kama siafu, yanaiteka kasri, yanamwua Mfalme Belshaza. (Danieli 5:30) Kwa usiku mmoja, ushindi wakamilika. Babiloni kaanguka, unabii katimizwa neno kwa neno.

  • Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Sababu Itakayofanya Yehova Ampendelee Koreshi

      8. Ni sababu gani mojawapo inayofanya Yehova ampe Koreshi ushindi juu ya Babiloni?

      8 Baada ya kutaja ni nani atakayeshinda Babiloni na atashinda jinsi gani, Yehova anaendelea kueleza sababu moja itakayofanya Koreshi apewe ushindi huo. Yehova anaongea na Koreshi kwa njia ya unabii na kusema kwamba sababu ni ili “upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA [“Yehova,” “NW”], nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” (Isaya 45:3b) Inafaa mtawala huyo wa serikali kubwa ya nne ya ulimwengu katika historia ya Biblia atambue kwamba ushindi wake mkubwa zaidi umetokea kwa kuungwa mkono na mtu mkubwa kuliko yeye—Yehova, Mwenye Enzi Kuu ya Ulimwengu Mzima. Inampasa Koreshi akiri kwamba yule anayemwita, au kumpa utume, ni Yehova, Mungu wa Israeli. Maandishi ya Biblia yanaonyesha kwamba kwa kweli Koreshi alikiri kuwa ushindi wake mkubwa ulitoka kwa Yehova.—Ezra 1:2, 3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki